Oktoba ya ule mwaka
Na.Mwanakalamu
Tanu wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba mwaka ule iikuwa ni wiki ngumu sana kwa baba, alikuwa habanduki kwenye redio hata pale nilipompigia kelele ama kumsumbua kwa namna yoyote hakuhangaika nasi bali alijitenga na kuingia chumbani.Shuleni tulikokuwa tukisoma , akifundisha baba alikuwa akijifungia ofisini kwake muda mrefu sana na redio yake.
Sikujua chochote kilichomfanya awe katika kupenda kusikiliza redio kwa kiwango kile huku akiwa mwenye hofu sana.Kwa umri wangu na elimu yangu ya darasa la kwanza nililokuwa nikisoma sikuona umuhimu wowote wa kujua kilichomsibu zaidi ya kuendelea na michezo ya kitoto kutwa japo usiku niliporudi nyumbani nilikuta akiwa amenyong’onyea sana ,nikawa naogopa sana lakini sijui ndo utoto wenyewe sikujihanganisha naye sana kwani upole wake pia ulikuwa ji nafasi yangu ya kutozingatuia maagizo yake.
Jioni ya tarehe kumi na tatu nakumbuka ilikuwa ji siku ya jumatano siku ambayo nilitakiwa kufua nguo zangu kwani siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya kukaguliwa usafi shuleni baba yangu alionekana mwenye hofu sana.Nilipata nafasi ya kuuliza juu ya hofu aliyokuwa nayo na kumfanya awe rafiki wa redio wakati akinifulia nguo za shule ambazo hadi usiku wa saa moja na robo baada ya habari ya sauti ya Tanzania Zanzibar.
Alinijibu kwa kifupi tuu;
‘’Hali yake imekuiwa mbaya sana’’
Nilipouliza ni nani huyo , hakunijibu zaidi ya kunizuia kuongea kwani kipindi cha michezo kilikuwa kimeshaanza, name nikaungana naye kusikiliza japokuwa nilikuwa sijui chochote zaidi ya kurithishwa ule ushabiki wake wa timu ya Simba.
Siku iliyofuata nilienda shuleni nikimwacha baba pale nyumbani akiwa mwenye hofu sana.Darasani tuliendelea na vipindi vya asubuhi hadi pale kengele ilipogongwa kwa dhalula.Walimu wote wakiongozwa na Mwalimu mkuu (baba yangu) akiwa mwenye uchungu mkubwa akitangaza kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nilimshuhudia baba yangu akilengwa na choxzi kabla ya kuondoka akijifuta machozi kwa kitambaa akimwacha msaidizi wake akimalizia matangazo na kututawanya akituambia tukawaaambie wazazi wetu tuu ya kifo hicho ya kiongozi huyo wa Afrika.Nakumbuka karibu darasa la kwanza wote tulianza kulia kwa sauti tukiwa hatujua kilichomliza mwalimu miuu na kuwafanya walimu wengine wawe katika simazi vile.Wanafunzi wa madarasa ya juu nao walianza kulia kwa sauti ya chini lakini wanafunzi wengi wa kike walilia kwa sauti kama tulivyokuwa tukilia darasa la kwanza.
Baba wa taifa amefariki kwa hiyo taifa litakosa mzazi, tutaishije tukiwa mayatima? Hilo lilikuwa swali la kwanza kichwani mwangu niwa njiani kuelekea nyumbali palipokuwa si mbali na shuleni (kumbuka tulikuwa tukikaa nyumba za shule).Nilimkuta baba akiwa ameshika tama redio ikitoa sauti yake Sauti ya mamlaka ya Rais mkapa iliyokosa nguvu ilisikika kila baada ya dakika chache ikirudiwa kutangazwa kifo cha Mwalimu Nyerere.
Hapo nikagundua kilichomfanya baba awe mnyonge kwa karibu wiki mbili huku redio ikiwa ni rafiki yake mkubwa , mama naye alikuwa akielekea jikoni aliponiona pale sebuleni nikimtazama baba aliyelengwa na machozi ya uchungu, nikaamua kumfuata.
‘’Mama unamjua baba wa taifa?’’Nilimuuliza tulipofika jikoni.
‘’Ndiyo ni kiongozi wa kwanza wa Tanganyika huru, huyo ni mwanamapinduzi halisi , mjaa wa kweli masikini Mungu amemchukua kabla hajawasuluhisha warundi’’Mama aliongea kwa uchungu mkubwa maneno ambayo kwangu yalikuwa mageni sana.
‘’Baba yako ni mfuasi wa ujamaa wa kweli kama alivyokuwa Mwalimu na hayati Sokoine ndiyo maana akakuitwa Moringe anaamini utakuwa ni lama na ukumbusho kwake’’
‘’Sokoine naye amefariki?’’Niliuliza nikimfuta mama machozi.
‘’Ndiyo kwa ajali tata ya gari’’Aliongea mama kwa kifupi akianza kuhangaika na sufuria aandae chakula ambacho hata baada ya kuiva hakikuliwa na yeyote wote tulikuwa na hofu na uchungu mkubwa.
‘’Mapebari watakuwa wamefurahi, watauvinja na Muungano wetu kama walivyolizika azimio la Arusha mbele ya mcho yake’’ Nilimsikia baba akiongea kwa kifupi na kuingia chumbani.
Hivyo ndivyo kifo cha mwalimu kilivyopokelewa kwenye familia yetu, niambie mlikipokeaje kwenu?
Kupata makala zaidi tembelea ukurasa wa Kalamu Yangu (Bofya hapa)
No comments