Habari mpya

Kituo chakulelea watoto waishio katika mazingira hatarishi Wilayani Ludewa chakabiliwa na changamoto lukuki

 Hiki ndicho kituo cha watoto waishio katika  mazingira hatarishi na wenye ulemavu wa ngozi wilayani Ludewa

Mkurugenzi mtendaji wa NICOPOLIS ACADEMY Bw.Augustino Mwinuka akisoma ripoti ya kituo hicho na changamoto zake 


viwanja vya watoto vya kituo cha NICOPOLIS ACADEMY 
Raia wa Ujerumani wakiwa na wenyeji wao katika kituo cha NICOPOLIS ACADEMY 
PROF; LUDWIG GERNHARDT  raia wa ujerumani akiwatambulisha alioongozana nao na kueleza dhumuni la msaada wake
Watoto wenye ulemavu wa Ngozi wanaotunzwa katika kituo hicho 
Mwenyeji wa Wajerumani hao Bw.Willybad Mwinuka akiwakaribisha wageni wake 
  PROF; LUDWIG GERNHARDT akitoa zawadi kwa watoto hao
Ngoma ya saili ya Mganda kutoka Boma la Mzalendo ikitumbuiza katika ugeni huo 




 Mkurugenzi wa kituo hicho na wageni wake wakifuatilia burudani kutoka katika vikundi vya ngoma


Kituo cha watoto waishio katika mazingira hatarishi na wenye ulemavu wa ngozi kijulikanacho kwa jina la NICOPOLIS ACADEMY PRE and PRIMARY ENGLISH MEDIUM SCHOOL kilichoko wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ambacho kinakabiliwa na changamoto kubwa ya fedha ya uendeshaji wa kituo hicho hivi karibuni kiliweza kutembelea na raia wa Ujeruman na kujua changamoto zao.


Akiwakaribisha wageni hao kutoka nchini Ujeruman ambao ni familia ya  Mkurugenzi PROF; LUDWIG GERNHARDT mtendaji wa kituo hicho Bw.Augustino Mwinuka alisema kuwa kituo hicho ambacho kinaonesha kuwa msaada mkubwa kwa jamii ya Ludewa kwa siku za mbeleni kimekuwa kikiendeshwa kwa michango ya wafadhiri wan je ya nchi na ndani japokuwa ni kidogo lakini hakuna namna.


Bw.Mwinuka alisema kuwa PROF; LUDWIG GERNHARDT  amekuwa msaada mkubwa kwani mpaka sasa kuna baadhi ya vitu ambavyo ameshakisaidia kituo hicho kama vile vitanda kumi double deck na magodoro yake,vitanda viwili vya watumishi na magodoro yake,meza mbili na viti vitano vya ofisini,viti ishirini vya wanafunzi.


Vifaa vingine ni blanket ishirini na mashuka ishirini ya wanafunzi komputa moja na modem moja,vitabu vyenye thamani ya shilingi laki mbili,kuku jogoo mmoja,mbuzi mmoja,mayai arobaini na nane na lita tano za Asali hivyo kukifanya kituo hicho kupata ahueni ya namna ya kujiendesha.


“Kituo chetu ni kichanga lakini ni msaada mkubwa kwa wanaludewa kwani mpaka sasa limeshakuwa kimbilio la wengi ingawa bado tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha za kununulia mahitaji kwaajili ya watoto hawa hivyo tunaiomba jamii kutuunga mkono kwani ni kituo pekee wilayani Ludewa kinachoendeshwa na watu binafsi na kwa michango ya wadau”,alisema Bw.Mwinuka. 


Bw.Mwinuka alisema kuwa uongozi wa kituo hicho umeamua kuanza ufyatuaji wa tofari kwaajili ya kujengea mabweni ya wanafunzi ndani ya mwaka huu kwani kituo kinatarajia kupokea wanafunzi zaidi ya 200 baada ya miaka miwili kwani uhitaji wa watoto kuomba nafasi katika kituo hicho ni mkubwa lakini wameshindwa kuwapokeakutokana na ukweli kwamba hakuna vyumba vya kuwalaza.


Mkurugenzi wa kituo hicho anawaomba wananchi na wadau mbalimbali kuchangia kwa hali na mali ili kuweza kukamilisha ujenzi wa mabweni hayo kwani watoto hao mpaka sasa wanaishi katika nyumba ya mtu ambako kituo kimelazimika kuikodi na kuiweka kama bweni la watoto hao.


Akiongea na wananchi pamoja na uongozi wa kituo hicho hivi karibuni alisema kuwa PROF; LUDWIG GERNHARDT  baada ya kuombwa msaada wa kuchangia kituo cha  NICOPOLIS ACADEMY aliguswa na changamoto wanazokabiliana nazo hivyo yeye na familia yake waliona ni vyema wakajitolea msaada huo.


PROF; LUDWIG GERNHARDT alisema kuwa imekuwa kawaida yeye kutoa misaada mbalimbali katika nchi ya Tanzania hasa wilaya ya Ludewa katika vikundi na shule mbalimbali lakini mara nyingine anavunjika moyo pale anapoona misaada hiyo haitumiki kama ilivyoombwa na walengwa.


Aliwaasa viongozi wa kituo hicho kutoshawishika na wengine wenye nia ovu na misaada ya wafadhiri badala yake waendelee kuwaomba wadau mbalimbali katika kuhakikisha watoto hawa wenye mazingira hatarishi na wenye ulemavu wa ngozi wanapata maisha bora hivyo ataendelea kuunga mkono juhudi hizo ambazo zimeanza vizuri na zinaonekana kwa macho.


Aidha mwenyeji wa Wajerumani hao nchini Tanzania ambaye ndiye alikuwa akiwatembeza maeneo mbalimba nchi Bw.Willbad Mwinuka alisema kuwa ugeni huo umekuwa ni ugeni wa Baraka kubwa wilayani Ludewa kwani ni miaka mingi hivi sasa wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali hasa katika kuwalipia ada za shule watoto wanaoishi mazingira hatarishi.


Bw.Mwinuka alitoa angalisho kuwa wale wote wanaopata misaada na vitu mbalimbali kutoka kwa Mjerumani huyo wanapaswa kufikishwa kwa walengwa kama vilivyo ili kumtia moyo mfadhiri kuendelea kuifadhiri wilaya ya Ludewa pia jamii inayoguswa na uwepo wa watoto hao inapaswa kujitolea na sio kusubiri kutoka kwa wenzetu wan je ya nchi kwani iko siku moja watasitisha kutusaidia.


Mwisho.


Mkurugenzi wa kituo  sim no 0765059184

No comments