Habari mpya

Siku 60 zilizotolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) kwa wadaiwa zafika ukomo. Kifuatacho ...

Siku ya tarehe 13 mwezi wa tatu mwaka huu bodi ya mikopo ilitoa tamko juu ya ulipaji wa mikopo kwa wanafunzio waliohitimu vyuo vikuu tangu mwaka 1994 juu ya urejeshaji wa mikopo hiyo. Tangazo hilo lilionyesha kuwa tamko hilo litaanza kufanya kazi siku iliyofuatia yaani tarehe 14 machi.
  1. Je, wamefanikisha kwa kiasi gani kukusanya mikopo hiyo kwa wadaiwa husika?
  2. Vipi kuhusu lengo lao la ukusanyaji wa bilioni nane kwa mwezi! limefanikiwa kwa kiasi gani?
  3. Na, je wadaiwa hao waliandaliwa kisaikolojia kuanza kulipa deni hilo kwa sasa kwa kipato wanachopata?
  4. Na wale wa sekta binafsi watarejesha kwa mtindo upi?
Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo nimekuwa nikijiuliza juu ya tamko hili ambalo inaonyesha limekuwa na utata kidogo kwa wadaiwa wenyewe kwani wengi wamekuwa wakilalamika juu ya hali ya maisha ya sasa ukilinganisha na kipato kidogo ambacho wamekuwa wakikipata. Pia ukiangalia kwa undani utagundua ni asimilimia ndogo sana ya wadaiwa wa mikopo hiyo wapo katika sekta binafsi na ajira zisizorasmi.

Kama hukubahatika kuliona tamko hilo la HESLB ifuatilie hapa ..

No comments