Habari mpya

Juma Kaseja, tajiri anayedakia Mbeya City (Sehemu ya mwisho)


Na.Mwanakalamu
Katika sehemu iliyopita  tuliishia pale nilipopata taarifa za kutoka katika kile kijiji cha Kaseja mtoto lakini  kuna kitu nilichomwahidi yule mtoto na kumfanya afurahi sana.
Ni kitu gani hicho?  Tuendelee na simulizi hii ya kuvutia.
Baada ya kuzunguka huku na huko katika siku ile  iliyokuwa ya mwisho katika ziara yangu  nikiwa na yule rafiki yangu nilifanilkiwa kugundua mambo mengi sana.Katika niliyokuwa nimeyagundua ni majina ya wachezaji wachache sana wa Tanzania yaliyoikuwa yakisikia midomoni mwa  watoto lakini mwengi yalikuwa ni majina ya wachezaji wa Ulaya na Amerika.
Palikuwa na akina Messi, Rooney, Mata, Ronaldo na wengine wengi huku majina machache kama Kaseja, Mwameja,Tegete, Ngasa na mganda Okwi.Lakini kulikuwa na kitu cha ajabu kidogo kwani fualana nyingi za timu za nh’ambo zilikuwa na majina na namba za wachezaji wakati wale waliokuwa wamejiita majina ya wachezaji wa Tanzania walikuwa  ama wameaandika kwa rangi za nyumba ama wamechora kwa wino wa peni  au walikuwa hawajaandika chochote.
Ilinisikitisha sana, lakini sikuwa na namna zaidi ya kuamini kuna siku nitatumia kalamu kuufikisha ujumbe wangu kwa matajiri hao wakitanzania waliokuwa wakiziacha fedha zikiishia kwenye mitumba kutoka Ulaya iliyopitia Malawi na Msumbiji.
Siku iliyofuata nilisafiri kwa pikipiki hadi nilipofika kwenye mji ambapo palikuwa na gari zilizonifikisha Mjini Songea ambapo kitu cha kwanza nilichokifanya ni kutimiza ahadi yangu kwa Kaseja Mdogo.Niliingia kwenye duka moja la vifaa vya michezo ambapo nilipata kununua raba za michezo za saizi ndogo ,bukta na fulana nyekundu na nyepe kasha nikaingia mtaani kwa wataalamu wa nembo na michoro ya nguo ambapo niliwaeleza waaandioke namba moja na jina la Juma Kaseja Mgongoni.
Yule jamaa aliniangalia usoni na kuanza kufanya kazi niliyokuwa nimemweleza huku akionekana kutaka kuongea kitu lakini alionekana kama kuniogopa hivi.
‘’Vipi mbona kama kuna kitu unataka kuongea?’’ Niliamua kumuuliza.
‘’Hivi unajua Kaseja anachezea mbeya City?’’ Alinijibu kwa swali.
‘’Naaam nalijua hilo’’
‘’Mbona umemnunulia jezi ya Msimbazi?’’
‘’Kaseja ni Simba na Simba ni Kaseja’’Nilimjibu.
‘’Hiyo ilikuwa zamani  siyo leo’’Aliongea kama akinikosoa vile.
‘’Hapa hadi leo kaseja ni Simba sema Simba hawataki iwe hivyo,Masabiki tunatamani hata awe mshauri wa timu hata kama hachezi, iwe tuu kama Drogba alivyorudio pale chelesea ama anavyofanya Mgosi pale Msimbazi’’Nilieleza kwa masikitiko kidogo.
‘’Lakini si kwa viongozi wale , viongozi waliamua kumwacha kisa tuu yeye ni maarufu na tajiri kuliko wao’’Ananidokezea kitu huyun jamaa huku akionekana kuachana na ile kazi ya kuchora a,anaonekana mwenye hasira.
‘’Kwa hiyo Kaseja ni tajiri sana?’’ Namuuliza nikiwa siamini kauli yake.
‘’Ndiyo ni tajiri na anaweza kuwa tajiri zaidi’’
‘’Kivipi?’’
‘’Unaambiwa Kaseja ana miradi mingi kawekeza huko , lakini bado ananafasi ya kuwa tajiri’’Ananieleza yule jamaa wakati huu anaendelea kuchora.
‘’Kivipi?’’Nalirudia swali langu.
‘’Unajua hapa ulivyonunua hii jezi na kuja kuichora kwangu , hela hii ilikuwa yake ila hajaamua kuwekeza huku’’
‘’Ila kweli’’Najibun na kusubiri aongee inaonekana ana mengi sana.
‘’Unaona hii?’’ Ananiuliza akinionesha kitu kwenye simu yake.
Ni video iliyowekwa na Kaseja kwenye ukurasa wake wa instagram , inamwonesha akishuka kwenye basi huku akishangiliwa na kundi kubwa la watoto na vijana.Hapo ananikumbusha siku moja alipokuja na timu yake ya Simba  mwaka 2010 pale Njombe ambapo watoto wato walianza kumshangilia  tangu aliposhuka kwenye basi, pale hotelini walipolala wachezaji watoto walikuwa hawabanduki wakimchungulia Kaseja wakiita jina lake, kumbuka kipindi hicho Simba ilikuwa pia na akina Okwi sijui Mgosi lakini Kaseja alikuwa kivutio cha kila mtu.
Uwanjani pale Sabasaba ingawa hakuanza kucheza watoto walikuwa kwa kaseja tuu si kwa timu iliyokuwa uwanjani.
‘’Hiyo ilikuwa Shinyanga, kila apitapo hali inakuwa hivyo, Kaseja ana nyota ya akina Diamond, Lowasa na Alikiba’’Ananieleza yule jamaa baada ya kunionesha picha kadhaa za kaseja alizokuwa ameweka kwenya akaunti yake.
Lakini alinionesha picha moja ambayo iliniumiza moyo wangu ,ilikuwa ni picha iliyomwonesha akiwa uwanja wa Taifa akishangilia kipindi hicho yupo Simba, chini yake kuna maandishi.
‘’WANASIMBA MNIKUMBUKE KWA MABAYA YANGU’’
Hiyo ilikuwa pia ni komenti ya picha iliyokuwa imetangulia baada ya dada mmoja kumwambia anatamani arudi Msimbazi, huyo dada alidai kuwa amekuwa shabiki wa Simba kwa sababu yake hivyo hata haoni umuhimu wa kuwa  Simba, alkini Kaseja alimjibu huyo dada kuwa yeye na wanasimba wenzake wamkumbuke kwa mabaya yake.Iliumiza kweli kipenzi huyu wa Simba aliyaongea ya moyoni mwake , ilionesha wazi kuna kitu hakikuwa sawa katika kuondoka kwake msimbazi ingawa anaonekana kuwa na mapenzi mema na timu hiyo.
‘’Hii ndo Tanzania’’Niliongea kwa kifupi.
‘’Lakini ana nafasi’’ yule jamaa ananiambia kwa kifupi akiiweka vizuriile fulana ambayo alikuwa amemaliza kuichora.
‘’Kurudi Simba?’’Nauliza nikiwa nimehamaki.
‘’Hapana sahizi mkataba wake na Mbeye City umeshaisha tangu muda sasa, lakini aliamua kuitumikia timu hadi  mwisho wa msimu, anaweza kuongeza mkataba ama kwenda timu nyingine na hata akikosa timu anaweza kuendelea na soka akiwa kama mkufunzi ama mhamasishaji  wa wanasoka chipukizi.
 Makampuni yapo mengi awashawishi tuu wanaweka mpunga na kuanzisha kakituo kakizushi kanakuwa ni chuo cha kuwanoa makipa ambao watakuja kuisaidia nchi na hata kuuzwa nje, haijalishi hata kama yeye hatowafundisha yeye waletwe tuu wataalamu wamsaidie huku akizunguka nchi zima mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, tarafa kwa tarafa kata kwa kwata na kijiji kwa kijiji.
Hapo anaenda kutafuta wataalamu na wabunifu wanabuni jezi rangi na muundo wake zinaandiokwa jina lake, anaweka sokoni viatu , gloves na vifaa vingine vya michezo kasha anapozunguka kutafuta vipaji basi huko pia anaweka vituo vyake ambako vifaa vyake vitauzwa huko.
Nakwambia Kaseja ni tajiri mkubwa sana hata asipocheza soka, na katika soko ukiachana na bidhaa za urembo wa wanawake vitu vya watoto vinanunulika sana angalia hata we mwqenyewe umeamua kumnunulia mwanao nadhani baada ya kukusumbua, watoto wakiona watakulilia mzazi na kama nawe hueleweki mtoto anaweza kuiba akaipate jezi full ya Kaeja Tanzania One , Tajiri anayedakia Mbeya City’’.
Anamaliza yule jamaa akinikabidhi jezi zangu ambazo nziweka kwqenye mfuko na kwenda kumpa rafiki yangu mwenyeji wa kule kijiijini mwambao wa ziwa nikimwomba amfikishie rafiki yangu Kaseja mdogo.
Kuna kitu nakikumbuka , naamchelewesha tena yule mwenyeji wangu kwa kuingia palipo na huduma ya intaneti naishusha picha kadhaa za Juma Kaseja na kuzichapa kwenye karatasi naiweka kwenye bahasha na kwenda kuunganisha na ule mzigo wa jezi.
Ninaagana na rafiki yangu kasha naenda uwanja mdogo wa ndege na kufanya taratibu za safari na baada ya saa chache najikuta nipo kwenye jiji la joto , jiji lenye timu ambayo Kaseja ameitumia kwa muongo mzima.
Dah! Huyu ndiye Kaseja tajiri anayedakia Mbeya City.
Niandikie maoni yako hapa  chini.

No comments