Maandalizi ya tamasha la Maji Maji Selebuka yazidi kupamba moto zikiwa zimebaki wiki mbili kuanza.
Maji maji Selebuka ni tamasha linaloandaliwa na Kampuni binafsi iitwayo Tanzania Mwandi ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Songea Mississippi (SO-MI). Shirika hili linahusika na mambo ya maendeleo ya jamii na elimu kwa wanaSongea kwa ushirikiano kati ya Songea Tanzania na Mississippi Marekani tangu lilipoanzishwa 2008.
Tamasha la Majimaji Selebuka 2016 linahusisha mambo yafuatayo;
- Mbio za nyika (Marathon)
- Mbio za baiskeli (Cycling)
- Ngoma za asili (Traditional Dances)
- Mdahalo wa shule za sekondari (Schools debate)
- Maonyesho ya ujasiliamali na biashara (Trade fair and entreprenuership)
- Utalii wa ndani (Local tourism)
Mwaka huu tamasha la Majimaji Selebuka litafanyika kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 04 Juni 2016 katika viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa wa vita vya majimaji mjini Songea katika mkoa wa Ruvuma Tanzania.
Tamasha hili linafanywa kwa lengo la:
- Kuibua vipaji na kuviendeleza kupitia michuano ya kimichezo. Kutakuwa na mashindano ya Mbio za Nyika(Marathon) 42km, 21km, 10km na 5km(Run for fun), na Mbio za baiskeli ambazo tunaamini kwa mwaka huu zitakuwa za aina yake kwa sababu tunategemea kupata washiriki wa mbio za baiskeli kutoka nchi za jirani kama Rwanda.
- Kuibua na kutambua fursa za kiuchumi hasa kwa wajasiriamali wa mkoa wa Ruvuma kupitia maonyesho ya shughuli za wajasiriamali pamoja na biashara katika viwanja vya Makumbusho ya vita vya majimaji kwa siku saba mfululizo kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 04 Juni 2016. Lengo likiwa ni kupanua soko la wajasiriamali kwa watu tofauti kwani kutakuwa na wageni mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi.
- Tamasha pia linalenga kuiendeleza elimu kupitia midahalo wa shule za sekondari.Katika kipengele hiki wanafunzi kutoka shule mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma, watapata nafasi ya kuchuana katika mdahalo ulioandaliwa na waratibu wa tamasha hili la Majimaji Selebuka. Mdahalo utafanyika tarehe 01 mpaka tarehe 02 Juni, 2016.
- Pia tamasha linalenga kuibua fursa za kiutalii zanazopatikana mko wa Ruvuma kupitia Utalii wa ndani.
Tutaanza tamasha kwa Mbio za Nyika (Marathon) ambazo zitafanyika siku ya ufunguzi tarehe 28 Mei 2016 kuanzia saa 12 asubuhi. Na tutafunga dimba kwa Mbio za baiskeli siku ya kilele cha tamasha la Majimaji Selebuka tarehe 04 Juni 2016. Ulinzi na usalama utakuwepo wa kutosha hivyo watu wasiwe na wasiwasi juu ya hilo.
Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi watakaoshiriki katika Tamasha la Majimaji Selebuka 2016. Kama vile Medali, Vikombe, Ngao, Vyeti,Fedha taslimu pamoja na zawadi nyingine kutoka kwa wadhamini wa kila tukio. Lakini pia kwa washindi watatu wa mbio za baiskeli watapata nafasi ya kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya mafunzo ya mbio za baiskeli za kimataifa.
Kwa sasa fomu za ushiriki zinapatikana kwenye tovuti yetu ambayo niwww.somi.international kwenye kipengere cha ‘DOWNLOADS’ hivyo basi kila mtu popote alipo anaweza kuingia na kuzichukua mda wowote anaotaka yeye.
Ada ya kushiriki katika tamasha itakuwa kama ifuatavyo;
- Mbio za Nyika (Marathon); 42km – 10000/=, 21km – 5000/=, 10km – 3000/= na 5km(Run for fun) - Bure
- Mbio za baiskeli; 50km – 10000/=
- Ngoma za asili; kila kikundi – 10000/=
- Maonyesho ya ujasiliamali; Kikundi – 50000/=, Mtu mmojammoja – 10000/=
Kwa maelezo zaidi tafadhari tembelea website zifuatazo;
Imeandaliwa na;
Reinafrida M Rwezaura
No comments