Awamu pili shindano la SBL kutafuta DJ mbobezi kuchanganya muziki yaanza
· Kuibua vipaji vya ndani
Dar es Salaam, Novemba 17, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuanza kwa awamu ya pili ya miezi mitatu ya shindano la kutafuta DJ aliyobobea katika kuchanganya muziki ambalo linalenga kuibua na kukuza vipaji vilivyomo ndani ya sekta ya muziki Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutambulisha awamu ya pili ya shindano hilo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Masoko na Vinywaji vikali wa SBL , Stanley Samtu alisema kuwa shindano hilo linadhaminiwa na kinywaji cha Smirnof Black Ice linamaanisha pia kuwapa wapenzi wa muziki kote nchini fursa ya kufurahia vibao vipya vya muziki vitakavyochezeshwa na ma+DJ walio na vipaji katika sekta hiyo.
“Leo tunatangaza ma+DJ 18 kati ya 40 kutoka mikoa mine ambao wamefanikiwa kuingia katika awamu ya pili ambapo Dar es Salaam wapo 10, Dodoma wawili, Arusha wawili, Morogoro wawili na Mwanza wawili,” alisema.
Kwa mujibu wa Samtu ni kwamba Smirnof Black Ice ni chapa ya kinywaji inayoongoza katika kipengele cha kinywaji maarufu miongoni mwa watumiaji wa tabaka la kati, katika maeneo yaote ya mijini na vijijini.
Tunaamini kwamba kupitia shindano kupitia shindano hili SBL itatoa vipindi vya kufurahisha miongoni mwa wapenzi wa muziki watakaotembelea yatakakofanyika mashindano na wakati huo huo kuwapatia fursa ya kipekee ya kuibua, kukuza na kuangalia vipaji vilivyopo katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ.”
Alisema kwamba kundi la vipaji vinavyosakwa katika mashindano hayo ni la vijana walio na umri kati ya miaka 18 hadi 30, ambao kwa mujibu wa Samtu ni kwamba shindano hilo linawafaa wanafunzi walio katika ngazi ya eilimu ya juu pamoja na wanataaluma ambao ni vijana. vijina.
“Zitatolewa zawadi nzuri kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kudokeza kuwa zawadi hizo ni pamoja na seti ya vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato, na mashine ya kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakafika fainali.
“Tunatoa wito kwa kwa ma-DJ wote , wasimamizi wa mabaa na wapenzi wa muziki katika miji hii kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia ili waweze kuifurahia sekta ya muziki ya Tanzania,” alisema Samtu.
Mwisho
No comments