SBL yatoa elimu kuhusu unywaji pombe kistaarabu Mkoani Dodoma
Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, akitoa semina elekezi kuhusu kampeni unywaji kistaarabu kampeni ambayo imezinduliwa mapema leo katika Hotel ya Morena mkoani Dodoma |
Wadau mbali mbali kutoka mkoa wa Dodoma wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni ya Unywaji kistarabu uliofanyika mapema leo Morena Hoteli Mkoani Dodoma. |
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya unywaji kistaarabu |
Dodoma , Novemba 9 , 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua
kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu.
Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua
changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mwakilishi wa Mkuu wa Usalama
wa Barabarani wa Mkoa wa Dodoma CP Steven Nchai, amesema kulishirikisha jeshi
la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL
wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na
uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na
kujiingiza katika ulevi wa kupindukia bila kuzingati vyombo vya moto
wanavyoendesha.
“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita
kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe
peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi”
aliongeza Nchai.
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya
zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala
yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria
zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa
pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Nchai.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia CP Nchai anasema
“ama kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la
kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba
wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya
kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana
wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya
pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali
wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha,
amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu
kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili
mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na
uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza
kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama
marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.
No comments