SBL yamzawadia mteja wa bia ya Pilsner pikipiki mpya
Meneja Chapa wa Bia ya Pilsner, Isamba Kasaka akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi wa pikipiki mpya iliyotolewa kwa Shindano la kunywa bia ya Pilsner lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki linalojulikana kama “Pilsner Lager Nguruma Party.” Pembeni yake ni Meneja Biashara Mipango na matukio Pwani na Dar es salaam Lulu Mduma katika hafla iliyofanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo. |
Dar es Salaam, Novemba 21, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetoa zawadi ya pikipiki mpya yenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa mkazi wa jijini Dar es Salaam aliyeibuka kuwa mshindi wa shindano la kunywa bia ya Pilsner lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki linalojulikana kama “Pilsner Lager Nguruma Party.”
Akizungumza katika mkutano wa waanndishi wa habari alipokabidhi zawadi hiyo Meneja Chapa wa Bia ya Pilsner, Isamba Kasaka aliielezea pikipiki hiyo kama zawadi kubwa kufuatia kuwepo kwa matukio mfululizo ya promosheni yanayofanywa na kampuni hiyo katika maeneo tofauti yanayotumika kwa vileo jijini.
“SBL imekuwa ikiendesha maonesho ya burudani ya bia ya Pilsner Lager katika mabaa yaliyoteuliwa ndani ya jiji ikiwa na lengo la kuwashukuru na kuwazawadia wateja wake wa bia hii. Katika mashindano, tumekuwa tunawauliza kuigiza mngurumo wa Simba na hatimaye mshindi anachanguliwa na wateja wenyewe,” alisema Kasaka.
Meneja wa bia hiyo alibainisha kuwa zawadi nyingine kadhaa zinatolewa wakati wa matukio hayo miongoni mwake zikiwa ni pamoja na fulana za Pilsner (T-shirts), bia za Pilsner za bure, Skafu za Pilsner (bandanas). Alisema kuwa tukio hilo limekuwa linahusisha maonesho mubashara (live) kutoka kwa wasanii wa ndani na kuongeza, “yote hayo ni katika kuwaongezea hamasa wateja wetu ili kufurahi na kuburudika.”
Naye mshindi huyo, Simon Jonas aliishukuru SBL kwa zawadi hiyo na kutoa wito kwa wanywaji wa bia waendelee kuifurahia Pilsner ili waweze kupata nafasi ya kutimiza ndoto yao ya kuendesha pikipiki kupitia promosheni.
Pilsner ni moja ya bia maarufu nchini na kote Afrika Mashariki. Bia hiyo ilizalishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1842 mjini Pilsen Jamhuri ambako ilipata jina lake ikiwa na kilevi cha asilimia tano. Bia hiyo kwa bei ya rejareja ni shilingi 1,600 kwa chupa ya mililita 500 na hivyo kuifanya wateja wengi kumudu kuinunua.
Mwisho
No comments