Habari mpya

Je, Utaku na kipi? Waza upya!


Na, ankali Ulamaa.
Watu hufa na vingi, wengine hufa na aibu zao, wengine hufa na sifa zao kutegemea na yale waliyoyafanya kabla hawajafa. Sijui wewe unadhani kwamaisha unayoishi utakufaje. 

Najua unamengi kichwani kwako, una ndoto nyingi tena ndoto kubwa, sijui unamipango gani kuhakikisha ndoto hizo zinakuwa halisi na watu wanaokuzunguka na kuishi nawewe wanaziona ndoto zako. 

Haisaidii kitu kuziongea tu ndoto zako kwa kinywa pasipo watu kuziona, kesho ukifa watu watasahau maneno yako lakini wanaweza kuvikumbuka vile ulivyovifanya hususan kama vimeyagusa maisha yao. 

Jitahidi sana usife na ndoto zako bali ufe na kumbukumbu za yale uliyoyafanya. 

Die with memories not with dreams









No comments