Mke wa aliyekuwa Raisi wa Kenya Mh. Mwai Kibaki afariki dunia
Na, Kaozat.
Mke wa aliyekuwa Raisi wa awamu iliyopita aliyemaliza muda wake nchini Kenya Mh. Mwai Kibaki amefariki dunia nchini Uingereza ambako alikuwa huko kwa ajili ya kupata matibabu katika hospitali ya Bupa Cromwell. Taarifa hiyo imetolewa na Raisi wa sasa wa Kenya Mh. Uhuru Kenyatta na pia imetangazwa na Televisheni ya KTN ya nchini Kenya.
Marehemu Lucy Kibaki (76) alizaliwa mwaka huko Mukurwe-Ini, Nyeri na kuolewa na Kibaki mnamo mwaka 1962. Katika maisha yao ya ndoa walifanikiwa kupata watoto wanne (4) Judy Kibaki, Jimmy Kibaki, Tony Kibaki, David Kibaki.
Umaarufu mkubwa aliojizolea Bi Lucy ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuwasaidia watu wenye mahitaji muhimu katika jamii kama walemavu na wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, AMEN.

No comments