Habari mpya

Sugu - Freedom (Official music video)

Mbunge wa Mbeya mjini ambaye ni msanii wa kitambo wa hiphop Tanzania Joseph Mbilinyi (Mr. II Sugu) aliahidi wiki kadhaa zilizopita kwamba ataachia video yake mpya baada ya kimya kirefu kwenye bongofleva, hii inaitwa ‘Freedom‘ ikiwa ni kazi ya mikono ya MJ Records.

Ndani wameonekana mastaa kadhaa wa bongo akiwemo Roma Mkatoliki, Producer Master J na Profesa Jay ambapo Mr. II kaiwakilisha Mbeya vizuri kwa kuvaa jezi ya Mbeya City Football Club pamoja na kofia yenye chata ya Mbeya. 

No comments