|
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
|
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akifungua moja ya bomba katika kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. |
|
|
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia) akifungua bomba katika moja ya kisima katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo pembeni yake ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. |
|
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mtinko katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi. |
Singida, Aprili 27th 2016: Kampuni ya simu ya Tigo leo imekabidhi visima 12 vya maji vyenye thamani ya 174m/- kwa vijiji 12 mkoani Singida ikiwa ni kuchangia juhudi za serikali za kupunguza uhaba wa maji safi na salama uliopo nchini.
Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye kijiji cha Mtinko wilayani Singida mkoani Singida, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata alisema ufadhili huo umo kwenye mikakati ya kampuni ya kusaidia jamii katika kunyanyua hali zao za maisha.
Vijiji vitakavyonufaika kutokana na ufadhili huo pamoja na wilaya zake kwenye mabano ni Lulumba (Iramba), Kisana (Iramba), Kisonzo (Iramba), Songambele (Iramba), Kinyeto (Singida Vijijini) na Damankia (Ikungi). Vingine ni Muungano (Ikungi), Ighuka (Ikungi), Kamenyanga (Manyoni), Sasajila (Manyoni), Mtinko (Singida Vijijini) and Kinampanda (Kinampanda).
“Msaada huu ni sehemu ya uwekezaji wa Tigo kwenye miradi ya kijamii ambayo inaleta tija kubwa kwa jamii. Tuna imani kwamba kupitia visima hivi, Tigo inasaidia kutatua uhaba mkubwa wa maji katika eneo hili la mkoa wa Singida ambalo kwa kiwango kikubwa limekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua katika kipindi cha miaka mine iliyopita,” alisema Lugata.
Aidha aliongeza kuwa uhaba wa maji miongoni mwa wilaya nyingi za Singida umesababisha wakiazi wake kupoteza muda mwinmgi kutafuta bidhaa hiyo muhimu, jambo ambalo Tigo inaamini kuwa hivi sasa litafikia ukomo kutokana na upatikanaji wa visima hivyo.
Makabidhiano ya visima hivyo yalihudhuriwa na kushuhudiwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye aliishukuru Tigo kwa ufadhili huo uliopatikana kwa wakati mwafaka akisema kwamba visima hivyo vitapunguza kwa kiwango kikubwa uhaba sugu wa maji uliolikumba eneo hilo na kuchangia kukua ustawi wa jamii kijamii na kiuchumi.
Hata hivyo, alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuchangia kwenye juhudi kama hizo. Waziri Lwenge alisema, “Tunatoa shukrani za dhati kwa Tigo kwa kutuunga mkono kwenye juhudi zetu za kutatua uhaba wa maji uliopo Singida na hata kwenye mikoa mingine nchini. Tuna imani visima hivi 12 vitasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili linaloikabili jamii kwa sasa”.
No comments