Habari mpya

USHAIRI KUTOKA KWA MORINGE JONASY MHAGAMA: MIE SINA NDUGU DAR

MIE SINA NDUGU DAR

Likizo yakaribia,tupo tunajiandaa,
Kila kona nasikia,wengi wataenda daa,
Eti watatembelea,bahari kuishangaa,
Nami najifikirisha,kweli sina ndugu dar.

Mawazo nayabadili,ludewa sikutamani,
Namwomba dada nauli,sitaki kwenda nyumbani,
Kichwani nina maswali,dar naenda kwa nani,
Leo nimeshagundua,mie sina ndugu dar.

Mori niende ziwani,si lazima baharini,
Kulala vibarazani,bora si nipo jijini,
Foleni barabarani,kuliko kutwa shambani,
Mori sina ndugu dar,najiendea nyumbani.

Utaenda kutalii,si leo badae sana,
Kiibiwa wala hulii,kikazana kusoma,
Ni tabu sikitanii,darwatu wabanana,
Wote mna ndugu dar,mie nataka kuanza.

Eti jiji la maraha,wengi wamo taabuni,
Wengi kwao karaha,hasa wale masikini,
Nitaomba msamaha,mlalao sebuleni,
Mie sina ndugu dar,mwenzangu upo kwa nani?

Nijibu uniambie,waweza kunipokea,
Nikija usikimbie,si jiji umezoea,
Ukweli uniambie,au nawe wazamia,
Mie sina ndugu dar,rafiki upo kwa nani?

KAMA DAR NDIO KWENU NIKARIBISHE NIJE PASAKA

Imetungwa na Moringe Jonasy Mhagama

No comments