Habari mpya

Washiriki kutoka Rwanda na Burundi wapigana ndani ya kijiji cha Maisha Plus.






Katika hali isiyotarajiwa katika kijiji cha Maisha Plus, jana washiriki wawili, KAREKEZI Jean kutoka Rwanda na BASWARI Nibigira kutoka Burundi walipigana hadharani huku wakirekodiwa na camera zilizofungwa kijijini hapo. 

Ilikua hivi;

SOLANGE kawakuta KAREKEZI na PATRICK wamekaa wanapiga stori akawaambia kwamba BASWARI alikua anamsema KAREKEZI kwa watu. 

KAREKEZI hakuonyesha kufurahishwa na ile hali, akapata hasira, PATRICK akachochea, akamwambia asikubali kudharauliwa, lazima akapigane. 

"Muacheni, kwani nyie hamjui BASWARI anavyojifanya anajua kila kitu?" SOLANGE akahoji.

PATRICK akaendelea kushauri kwamba KAREKEZI asikubali kuliacha liishie hapo.. Akampige BASWARI. 

Baada ya kuona KAREKEZI anashawishika kwenda kupigana 
SOLANGE akamzuia asiende ili isijulikane kwamba yeye ndio ameleta hizo taarifa. 

KAREKEZI akiwa amekasirika akasema, "Mimi sipendi dharau... awe anawadharau nyie wanawake sio sisi wanaume." 

PATRICK akazidi kuchochea.. 'Nenda kampige asituchukulie hivyo... Kwanini atuseme vibaya?'

SOLANGE: "Usimdanganye mwenzio aende kupigana... Be gentle, men can't act like that... be gentle..''

Baada ya kuona mambo hayataishia pale, SOLANGE akaomba wasiseme kama yeye ndio ameleta hayo maneno.

KAREKEZI akamfuata BASWARI. Akamshika. BASWARI naye akamshika. Wakavutana. KAREKEZI akamwambia BASWARI, "Usiwe unaingilia maisha yangu, haunijui, wala sipendi unavyonisema kwa watu..." 

KAREKEZI akamtukana BASWARI kwa kifaransa. 

Ugomvi ukaendelea kwa muda.

SOLANGE akakasirika akatoka eneo la tukio akaona kama amesalitiwa... "Kwanini umenifanyia hivi, watu wakijua mimi ndio nimesema hayo maneno nitakua na bad image kwenye society.."

"Unaharibu reputation yetu kwa kugombana kijijni."

BABU hapendagi Ujinga. Kuna kikao cha kijiji asubuhi hii. Mjadala mkali unaendelea juu ya hatima ya hawa washiriki. Tukutane Azam Two saa 3.30 usiku kujua kitakachojiri. 

#VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu

No comments