Habari mpya

TASWIRA;KISHINDO CHA TIGO FIESTA KILIVYOFIKIA JIJI LA TANGA IJUMAA HII

Roma Mkatolili akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta katika Tamasha hilo liliofanyika katika viwanja vya  Mkwakwani Jijini Tanga usiku wa Ijumaa .
Nahreel na Aika toka Kundi la Navykenzo wakilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta katika viwanja vya Mkwakani Jijini Tanga

Shetta akiwa na wacheza wake akitoa burudani kwa maelf ya mashabiki waliojitokeza  katika Viwanja vya Mkwakwani usiku wa Ijumaa 

Kundi la weusi wakitoa burudani na michano ya nyimbo zao kali kwa wapenzi wa muziki waliojitokeza katika Tamasha la burudani la Tigo Fiesta jijini Tanga
 Barnaba akiwa  kwenye  jukwaa la Tigo fiesta uwanja  wa  Mkwakwani   Tanga  usiku  wa  ijumaa hii

Benpol akitumbuiza kwa Style ya Mduara na wacheza shoo wake 

DOGO JANJA naye akiwakonga wapenzi wa muziki waliojitokeza katika Tamasha la Tigo fiesta

Makomandoo wakionesha umahiri wao wa kumiliki jukwaa 



Maua Sama naye aliwakonga nyoyo wapenzi wa burudani waliojitokeza kwa wingi katika Tamasha la Tigo Fiesta jijini Tanga


Nay wa Mitego akilivamia jukwaaa la Tigo Fiesta katika Tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya Mkwakani usiku wa ijumaa wiki hii



Maelfu ya wakazi wa jiji Tanga waliojitokeza katika viwanja vya Mkwakwani katika Tamasha la Tigo Fiesta wakipata burudani kwa wasanii wa Bongofleva na Vikundi vya Taarabu vilivyotoa burudani ya kukata na shoka usiku  wa ijumaa.

No comments