|
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiongea na waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games jijini Dar Es Salaam jana.Tigo Games ni huduma katika wavuti ambayo imesheheni michezo mingi kwa ajili ya wateja wa Tigo wenye simu za Smartphone au Tablet zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakua App ya Tigo Games.
|
|
Wasanii wakiigiza kama Mazombie katika kunogesha uzinduzi wa TIGO GAMES |
|
Wasanii wakicheza mpira katika uzinduziwa tigo games mapema jana katika ukumbi wa High Spirit Jijini Dar es salaam |
|
Wadau mbalimbaliwakipata taswira mbele ya gari katika RED carpert |
|
Wasanii wakiwa katika pozi na mfano wa Risasi katika uzinduzi wa TIGO GAMES |
|
Wadau wakifurahi jambo katika uzinduzi huo |
|
Mtangazaji wa Choice Fm na Mchekeshaji Idris Sultan akiwa live jukwaani kusherehesha uzinduzi wa Tigo Games mapema jana katika ukumbi wa High spirit Jijini Dar es Salaam |
|
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akifurahi jambo na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kushoto ) wakati wa uzinduzi |
|
Wasanii wakitumbuiza nyimbo za michael Jackson |
|
Mfanyakazi wa Huawei akielekeza jinsi ya kucheza Games hizo mbalimbali zinazopatikana katika Tigo Games |
|
Baadhi ya wadau wakipata maelekezo jinsi ya kuingia katika mashindano ya kucheza Games na mshindi kujishindia Zawadi |
|
Waadndishi wa habari wakishindana kucheza Games katika uzinduzi wa Tigo Games jana usiku |
|
Msanii wa kizazi kipya Benpol akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa clouds tv Perfect baada ya uzinduzi wa tigo games |
|
Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Tigo Games mapema jana usiku |
|
Wadau wakipata picha katika sanamu za michezo ya Tigo Games |
|
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Tigo Games |
Dar es Salaam, Mei 19, 2016- Kampuni
ya simu inayoendesha maisha ya kidijitali Tanzania, Tigo, leo imetangaza
uzinduzi wa huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games. Tigo
Games ni huduma katika wavuti ambayo imesheheni michezo mingi kwa
ajili ya wateja wa Tigo wenyeSmartphone au tablet zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakuaApp ya
Tigo Games. Kwa wateja wenye simu
za kawaida zilizo na intaneti watapata huduma hii katika tovuti ya Tigo Games.
Michezo zaidi ya 800
inapatikana kupitia huduma hii ikiwemo
michezo maarufu ambayo ni pamoja na Buddy Man, Cut the Robe,
Zombie Run na Tokyo Drift.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa huduma hii mpya jijini Dar es Salaam,
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “ Huduma hii mpya ya
michezo inaifanya Tigo kuwa ya kwanza katikamitandao ya simu Tanzania kutoa jukwaa la
michezo linaloweza kutumiwa na watu wengi ambapo wateja wa Tigo
wanaweza kucheza michezo mbalimbali kulingana na chaguo lao kwa
gharama wanayoimudu. Tigo imejikita kuendelea kusimamia
maslahi ya wateja wake kwa kutoa bidhaa nyingine nyingi kwa ajili
ya manufaa ya kuwa na simu za kisasa.”
“Tigo sasa ndio inaongoza
katika upatikanaji wa huduma ya 4G LTE nchini, na kwa sasa huduma hii
inapatikana katika miji mikubwa 12. Tunaamini
kwamba wateja wetu watafaidika sana kutokana na intaneti yenye kasi zaidi
itakayo wawezesha kupakua na kucheza michezo hii,” alisema Gutierrez.
Tigo Games ni huduma ambayo mteja akichajua kulipia mara moja, ataweza kuchagua michezoaipendayo na
kuicheza atakavyo wakati wowote.
Kuna VIP Club ambayo inampa mteja uamuzi wa kujiunga na kifurushi
cha siku, wiki na hata mwezi; pia
kinamruhusu mteja kupakua michezo bila kikomo.
Mteja ataweza kucheza michezo kwa mda
wowote autakao bila makato yeyote. Malipo
ya utumiaji wa data kadri mteja anaendelea kucheza ndio yatakayo hitajika. Uzinduzi
wa VIP Games Club utakapofanyika, siku 7 za mwanzo wateja wataweza kufurahia
huduma bure kwa kutembelea wovuti huu: http://burudani.tigo.co.tz/games
“Kuanzishwa kwa bidhaa
hii kupo kwenye mikakati ya Tigo ya kuwapatia wateja wake
bidhaa na huduma zilizo na ubora duniani ambazo zinawawezesha
kufurahia kwa ujumla maisha ya kidijitali,” alisema Gutierrez.
No comments