KUSUKA AU KUNYOA ROBO FAINALI MABINGWA ULAYA RAUNDI YA PILI
Usiku wa ulaya unarudi tena leo pale ambapo miamba ya soka barani ulaya itachuana katika robo fainali raundi ya pili ili kupata timu zitakazofuzu kuingia hatua ya nusu fainali.
Real Madrid wanatakiwa wafunge zaidi ya magoli mawili kwa bila ili kuindoa Wolfsburg katika mashindano hayo.
Rekodi zinaonesha ni timu mbili tu ziliwahi kuvuka baada ya kufungwa mechi ya kwanza ugenini kwa magoli mawili ikiwemo Real Madrid yenyewe pale ilipogeuza matokeo na kuifunga Red Star Belgrade 1987.
Kwa upande mwingine ushindani utakua kati ya Man.City ya England na PSG ya Ufaransa baada ya mechi ya awali kuisha kwa sare ya magoli 2-2 iliyofanyika nchini Ufaransa.
Hii hapa ratiba ya leo mechi za marudiano robo fainali mabingwa ulaya.

No comments