Kamata fursa: Tajirika kupitia kilimo cha Green House
 Hiki ni kilimo ambacho kinamuwezesha mkulima kudhibiti mazingira yake kwa maana ya nishati ya jua, unyevu na upepo.
 Wazo la kuzalisha mazao katika controlled environment lilikuwepo toka 
enzi za utawala wa Rumi na baadaye Green zilianza kuundwa na kufanya 
kazi karne ya 13 huko nchini Italia. Greenhouse imekuwa technolojia 
inayotumika katika nchi nyingi kuanzia Ulaya mpaka Asia, kumekuwa na 
project nyingi sana za Greenhouse na zimeonesha kuleta tija kubwa kwa wakulima.
 Greenhouse inamuwezesha mkulima kulima mazao hasa ya matunda na mboga. 
Greenhouse inamuwezesha mkulima kulima katika kipindi chote cha mwaka 
pasipo kujali misimu.
Ikumbukwe kuwa unaweza kuzuia magonjwa pia wadudu ambao ni hatari kwa mazao. Hili limeonekana kuwa na tija jwa magonjwa na wadudu ni changamoto kubwa katika kilimo ukiachilia mbali mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa.
Kabla ya kuamua kujenga Greenhouse unatakiwa kufanya utafiti katika udongo(soil pH, structure, texture &profile) ili ujue kipi cha kuongeza ama kupunguza. Pia unatakiwa kuchunguza aina ya maji na chemikali zilizomo ndani yake.
Kwa Tanzania bado inaonekana ni technologia mpya ila imekuwepo kwa muda sasa. Ukubwa wa Greenhouse unategemea na mahitaji yako pia mtaji ulionao. Kwa mfano material ya kujenga greenhouse y enye ukubwa wa 8m*15m hayazidi 3million, kwa ukubwa huu unaweza kuzalisha mpaka tan 30 za nyanya kwa mwaka na pia Greenhouse ina Guarantee ya kukaa miaka 10.
Imeandaliwa Na.Steven Mwakyusa
Chanzo: Kalamu Yangu

asante kwa elimu nzuri ni booonge la fursa
ReplyDelete