Habari mpya

Karibu Anthonio Conte lakini haya yanakuhusu,kibarua chako kinaanzia hapa.



Timu ya soka ya Chelsea ya Uingereza wametoa taarifa rasmi za ujio wa kocha wao mpya mtaliano Anthonio Conte ambaye anachukua nafasi ya kocha aliyefukuzwa Jose Mourinho lakini akipokea kazi kutoka kwa kocha wa muda Guus Hiddink.
Ujio wa kocha huyo unakuja na changamoto nyingi sio tu za kutwaa mataji na kucheza kwa kiwango cha juu lakini kwa jinsi atakavyokabiliana na mambo mbalimbali klabuni hapo.
Yafuatayo ni maswali mambo ambayo kocha huyo inabidi ayaweke sawa  kabla ya msimu mpya kuanza ili kuwa na timu bora .

1. Atampa mkataba mpya kapteni John Terry ambaye muda wake unaisha mwishoni wa msimu huu?

2. Ataweza kupandisha kiwango cha Eden Hazard au atamuuza kwa kwa kuwa anatakiwa na PSG na Real Madrid

3.Ataendana na sera za Chelsea za kununua  na kuuza wachezaji?

4.Atawapa nafasi za kucheza chipukizi?

5.Wachezaji wa mkopo kama Qudarado na wengineo atawarudisha?

6.Ataweza kuirudisha ligi ya mabingwa kwa kuwa ni dhahiri msimu ujao Chelsea haitashiriki  ligi hiyo enye heshima kubwa ulaya na duniani kote.

TUSUBIRI NA TUONE

No comments