Habari mpya

FULL TIME TANZANIA U17 vs MISRI U17.


Kati ya mechi ambazo msomaji hukupaswa kuzikosa ni kati ya Tanzania umri chini ya miaka 17 dhidi ya Misri umri chini ya miaka 17 kwani vijana wa Tanzania walipiga mpira sana.Mechi ya Leo imechezwa katika uwanja wa Azam complex Chamazi na kuoneshwa na Azam sports HD na Azam Two
Mechi ya kwanza vijana hao wa  Tanzania waliwafunga wenzao wa Misri kwa goli 2-1 na leo tarehe 5/4/2016 wamerudiana na matokeo na  ubabe umeendelezwa kwa vijana wa Tanzania kuwafunga tena vijana wa Misri magoli 3 - 2.
Tanzania walipata magoli yao kupitia kwa Ibrahim Abdalah aliyefunga magoli 2  Selemani Boko aliyefunga goli 1.
Umiliki wa Mpira Tanzania 49% - 59%
Mocha Bakari Shime wa Tanzania U17 (Serengeti Boys) anapaswa apate sapoti ya wadau na serikali kwa ujumla ili kuendeleza na kuthamini mchango wake.

No comments