Habari mpya

Fastjet yatoa zawadi shindano la Pasaka















Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

JUMLA ya washindi 12 wamepewa tiketi za bure za safari ya ndege katika shindano lililodhaminiwa na Festjet Tanzania.

Tiketi hizo ambazo zitawawezesha kusafiri katika ndege ya garama nafuu ndani ya ndani na nje ya nchi ambako Fastjet husafiri, ni sehemu ya zawadi zilizotolewa na kampuni ya Fastjet wakati wa msimu wa sherehe za Pasaka ziliyomalizika wiki iliyopita.

Akizungumza wakati wa sherehe ya kutoa zawadi hizo hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Afisa Uhusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro alisema kuwa shirika la Fastjet limechukua hatua ya kudhamini wateja wake kwa kuwapa zawadi hizo za tiketi za bure ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kurudisha shukrani kwa wateja wake ambao wamekuwa watiifu kwa shirika hilo.

“Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kampuni ya fastjet imekuwa ikitoa huduma bora za safari ya anga ambazo ni salama, zenye uhakika na kuaminika kwa wateja wake ambao hadi sasa wamefikia abiria milioni 1.8”, alisema Mbogoro.

Aliongeza na kusema kuwa, “tunaimani kubwa na wateja wetu kwa ushirikiano wao waliouonyesha pamoja na sisi katika kipindi hicho chote na kutokana na hali hiyo, fastjet imeamua kutoa zawadi ya tiketi za bure kwa baadhi yao ili wasafiri kwenda kokote kule ndani na nje ya nchi”, Mbogoro aliongeza.

Alisema kuwa tiketi hizo zitawawezesha washindi wao kusafiri na wenzi wao ili kufurahia msimu huu wa sikukuuu ya pasaka na wapendwa wao wakiwemo marafiki na jamaa zao.
Aliongeza kuwa, washindi hao walichaguliwa baada ya kutoa majibu sahihi wakati wa maswali yaliyofanyika kwa njia ya mahojiano ya vyombo vya habari nchini.


“Washiriki katika shindano hili walikuwa wengi mno, na kati yao 12 pekee ndio waliofaulu na jopo la majaji kuwachagua kama washindi”, Mbogoro alifafanua.

Katika mahojiano, mmoja wa washindi wa zawadi hii, Ally Sangawe, alisema: “ Naishukuru fastjet kwa kuandaa shindalo hili kwa kuwa sasa nitaweza kusafiri kwa kutumia tiketi hii ya bure na kufurahia wikiendi njema na mpenzi wangu. Hii ni fursa ya kipekee na ambayo ni muhimu kwangu”.

Karim Lungu, ambaye pia ni miongoni mwa washindi, alitoa rai ya furaha kwa waandaaji wa shindano hilo na kusema kuwa, “sasa kwa kuwa nilikuwa na hamu ya kusafiri kwenda Mwanza ambapo hapo awali sikuwa na uwezo wa kukata tiketi, na sasa nashukuru kupata tiketi ya bure ambayo sasa imeniwezesha kutimiza ndoto yangu ya kufika huko”.


Mbali na kusafiri ndani ya nchi kila siku katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya na Zanzibar, Mbogioro alisema kuwa Fastjet husafiri na kutua katika mji wa Johannesburg-Afrika ya Kusini, na pia kampuni ilizindua safari ya moja kwa moja kwenda Nairobi-Kenya na sasa imeongeza maradufu safari za kila siku, kutoka mara moja kwa wiki na kwenda mara mbili kwa wiki ndani ya miji hii miwili iliyo mikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

No comments