Alex Morgan, mwanasoka wa kike mwenye wafuasi wengi zaidi katika mitandao ya kijamii duniani
Social Media
2,667,696 Fans44,584 Talking About This
2,213,543 Followers
82.6 Klout Score
Alexandra Patricia "Alex" Morgan (Kuzaliwa, Julai 2, 1989) ni mwanasoka Mmarekani kutoka Diamond Bar, iliyoko katika jiji la California. Ni mmoja ya wachezaji wakubwa aliyebobea katika mambo ya soka na mwanachama wa timu ya soka ya wanawake, Marekani.
Morgan alikuwa ni mwanasoka mwenye umri mdogo zaidi katika timu ya taifa katika kikoso cha timu ya taifa ya wanawake iliyoshiriki kombe la dunia la wanawake mwaka 2011.
Umuhimu mkubwa wa Morgan ulionekana pale ambapo aliiwezesha timu yake ya taifa ya wanawake kuchukua ushindi katika kufuzu kucheza kombe la dunia la mwaka 2011, huko Ujerumani na kuifanikishia timu yake kuchukua medali ya shaba katika michuano hiyo mikubwa kabisa ya soka duniani. Pia kufanikiwa kushiriki katika michuano ya Olympic, London.
Baadae mwaka 2012, aliiwezesha timu yake kutoka kidedea katika michuano ya Olympic na kutwaa medani za dhahabu.
Alex Morgan akipambana vikali na Saki Kumagai wa Japani katika moja ya mechi ambayo Marekani ilitoka na ubingwa na kutwaa medali ya dhahabu |
Nje na soka Alex akishirikiana na Simon na Schuster wamefanikiwa kuandika kitabu kilichoongoza kwa mauzo na kushika namba saba kwa mauzo kilichoitwa "The Kicks" mwaka 2013, na kufuatiwa na maandiko mengine kama "Sabotage season" , kilichotoka mwaka 2013 pia.
Moja ya kitabu kilichoandikwa na Alex Morgan |
Imeandaliwa na Mr. Kaozat (kaozat1@gmail.com | 0655 987 588)
No comments