NAHODHA WA ZAMANI WA ENGLAND RIO GAVIN FERDINAND AAMUA KUSTAAFU SOKA
Ferdinand, mwenye Miaka 36, alimpoteza Mkewe Rebecca aliezaa nae Watoto Watatu hapo Mei Mosi Mwaka huu baada kuugua kansa na kufariki. Katika maisha yake ya Soka aliichezea Timu ya Taifa ya England mara 81 na pia kuwa Nahodha wake.Kwenye Klabu, Ferdinand alizichezea West Ham, Leeds United, Man United na kumalizia Msimu huu akiwa QPR ambayo imeshushwa Daraja toka Ligi Kuu England.Akiwa na Man United, Ferdinand alitwaa Ubingwa wa England mara kadhaa na pia UEFA CHAMPIONS LEAGUE pamoja na Klabu Bingwa ya Dunia.Akitangaza kustaafu, Ferdinand alitoa shukran kwa Mameneja na Wafanyakazi wa Klabu alizopitia pamoja na Familia yake na hasa Mkewe.
No comments