CHARLES MAKONGORO NYERERE ATOA SHUKRANI KWA WADAU MBALIMBALI WALIOJUMUIKA NA FAMILIA YA MAMA NYERERE KATIKA MSIBA WA JNDUU JON NYERERE
Kimekuwa
ni kipindi cha majonzi kwa familia ya Mama Nyerere baada ya kuondokewa
na kipenzi cha familia John Nyerere siku ya hivi karibuni. Kufuatia
kujitoa kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa bila kujali itikadi za vyama
vyao na watu mbalimbali kuifariji familia hiyo, Ndugu Charles Makongoro
Nyerere alikuwa na maneno machache juu ya upendo ulioonyeshwa na jamii
ya Kitanzania.
"Asanteni sana wote mliokuja kutufariji kama familia na wale mnaoendelea
kujaasanteni sana. Mwili wa marehemu John Nyerere, umeishawasili
nyumbani Msasani , heshima za mwisho zinaendelea kutolewa kwa mjibu wa
ratiba. Hatuna cha kuwalipa wote kwa kutufariji hata kwa ujumbe, mungu
awabariki sana."
No comments