Habari mpya

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA NA CHETI

Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu yatakayoanzaJanuari 2015 kama ifuatavyo:
KUNDI LA I
Waombaji wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya ualimu ambao waliwasilisha maombi yao Wizarani awamu ya pili kwa ajili ya kuchaguliwa kujiunga na mafunzo mwaka wa masomo 2014/15. Waombaji hawa wamechaguliwa na kupangiwa vyuo kulingana na Programu za mafunzo (Angalia orodha iliyoambatanishwa). Waliochaguliwa wanatakiwa kufanya maandalizi ya kujiunga na vyuo walivyopangiwa kwa kuzingatia maelekezo ya fomu zilizoambatishwa za kujiunga na chuo husika. Tarehe rasmi ya kuripoti vyuoni itatolewa mapema Januari 2015.

KUNDI LA II
Kukaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya ualimu mwaka wa masomo 2014/15 katika programu zifuatazo:
1.     Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Awali na Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi – Sayansi (Tarajali) (Miaka 3)
Wanaotakiwa kuomba mafunzo haya ni:
a)     Wahitimu wa kidato cha IV 2013 ambao hawakupata nafasi za kujiunga na kidato cha V katika shule za sekondari za Serikali mwaka wa masomo 2014/15. Orodha ya wahitimu husika imeambatishwa na tangazo hili (Angalia orodha iliyoambatanishwa).
b)      Waombaji wengine wenye ufaulu usiopungua Daraja la III katika mtihani wa Kidato cha IV uliofanyika kwenye kikao kimoja (single sitting) kati ya mwaka 2004 na 2013.

Mafunzo yatatolewa katika vyuo vifuatavyo:
a)    Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Awali
IlongaMhondaMtwara (K)Mtwara (U)SumbawangaKinampandaTarimeKatokeTandala, na Tabora.
b)   Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi – Sayansi (Tarajali)
TukuyuKasuluSongeaKorogweButimbaMpwapwaMorogoro, na Kleruu.
 2.     Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi -Walimu kazini (Miaka 2)
Wanaotakiwa kuomba mafunzo haya ni: Walimu Kazini shule za msingi (In-Service) ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ wenye uzoefu wa kazi usiopungua miaka 2 na  walio katika mpango wa mafunzo kwa mwaka wa masomo 2014/15 katika Halmashauri zao.

Mafunzo yatatolewa katika vyuo vya Bustani na Marangu.

Waombaji wenye sifa watume maombi yao kwa njia ya “Online” kwa kujaza fomu zinazopatikana kwenye Tovuti ya NACTE: www.nacte.go.tz.

Mwisho wa kutuma maombi ni terehe 31 Desemba 2014. Orodha za waombaji watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo haya na tarehe rasmi ya kuripoti vyuoni itatolewa mapema Januari 2015.


Imetolewa na:
KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
DESEMBA 2014

No comments