Habari mpya

BAADHI YA PICHA ZA GRADUATION YA MDAU WA BEST HOPE BLASIUS THOBIAS SIKU YA TUNUKU YA SHAHADA YAKE YA KWANZA

Kama kawaida timu nzima ya Best Hope hatupo nyuma katika suala la elimu na pale inapotokea mdau mkubwa kama bwana Ngambi kula nondoz lazima wadau wengine wajue kuwa kuna mwenzetu katunukiwa ili iwe ni chachu na kwa wadau wengine kuongeza juhudi katika mambo mbalimbali ili kuweza kufikia malengo waliojiwekea.
Ni furaha kubwa sana pale unapoona ndugu kutoka sehemu mbalimbali
wanakuja kushow love na kujumuika nawe katika siku muhimu kama hii.
Hapo ni Papaa Mchicha akiwa na Blasius Thobias katika siku ya kupokea
Shahada yake ya kwanza ya Sanaa ya Ualimu





Dada naye hakuwa nyuma katika kuonyesha furaha yake, naye alifika kutoa pongezi kwa mdogo wake

Add caption

Baada ya TUNUKU pozi la picha





Hapo chacha, when two Brothers met ndo mpango mzima hukamilika
mtu mbili kama milioni mbili kila kitu kwenye mstari. Hapo ni Master na Ngambi katika pozi
huku mpango mzima wa bata ukungojewa

Wazazi ndio waliotuleta duniani na kutuhudumia hadi kufikia hatua
kama hii, hapo ni Baba Mzazi wa Ngambi Bw. Thobias Lingalangala na ndugu
wengine wakijumuika katika siku hii muhimu kwa kijana wao

Pembeni kabisa kushoto ni Mh. Mtarajiwa Bw. Alisenus Mpangwa akijumuika na Ndugu kumpongeza kaka yetu

Sister na Uncle Perfect (aliyebebwa) walikuwepo pia kumpongeza Mdau Ngambi

TIMU NZIMA YA BEST HOPE NA NYASA PROFESSIONALS KWA UJUMLA WANAKUPA PONGEZI KUBWA SANA BWANA NGAMBI KWA KUFIKIA HATUA HIYO KUBWA SANA KATIKA MAISHA, MUNGU AKUTANGULIE NA KUKUZIDISHIA ZAIDI YA HAPO ILI UWEZE KUFIKIA MALENGO YAKO ULIYOJIWEKEA KWA MANUFAA YA FAMILIA NA JAMII NZIMA YA TANZANIA KWA UJUMLA.

1 comment: