PROFESA ANA TIBAIJUKA AKABIDHI RASMI ZAWADI YAKE YA TSH.9,500,000 MAMA SHUJAA WA CHAKULA, MAISHA PLUS
Mkurugenzi mtendaji wa DMB ambao ndio wamiliki wa Shindano la Maisha Plus Masoud Ally 'Kipanya' akiwa anaendelea kuendesha ratiba wakati wa Sherehe fupi za Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kukabidhi zawadi kwa washindi wa Mama shujaa wa Chakula pamoja na washiriki wote wa Maisha Plus 2014
Mgeni Rasmi Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akitoa Hotuba yake fupi ya kuwapongeza washiriki wote katika shindano la kumsaka Mama Shujaa wa Chakula na mpaka kupatikana mshindi, pamoja na kuwapongeza pia aliwaomba wakawe mabalozi wazuri kwa kwenda kuwafundisha wakulima wengine kile ambacho wamejifunza.
Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga akitoa Shukurani zake wakati wa Sherehe hizo
Mgeni Rasmi Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akimkabidhi zawadi ya Tsh 5,000,000 Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga kutoka Nansio Ukerewe Mwanza.
Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga kutoka Nansio Ukerewe Mwanza akionesha zawadi yake ya Tsh 5,000,000 aliyokabidhiwa na Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka
Afisa Mradi wa UKIMWI kutoka OXFAM Ester Mhagama akipokea zawadi ya Tsh 2,500,000 kwa niaba ya Mama Shujaa wa Chakula Msimu uliopita Sister Martha Mwasu kutoka kwa Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka
Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akimkabidhi David Sevuri zawadi ya Tsh 2,000,000 kwa ajili ya vijana wote walioshiriki katika shindano la Maisha Plus
"Wekeza kwa Wakulima wanawake wadogo wadogo Inalipa"
Mama Shujaa wa Chakula pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe ya Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kukabidhi zawadi yake rasmi.
No comments