HILI NDO ZALI JINGINE LILILOMWANGUKIA LADY JAYDEE, NI KUHUSU KOMBE LA DUNIA.
Msanii Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameula katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kupata nafasi ya kuandaa wimbo kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka duniani.
Jaydee anayefahamika pia kama Komandoo au Anaconda, amepata fursa ya kuandaa wimbo maalum wa michuano hiyo ‘FIFA World Cup Anthem’ akishirikiana na wakali wawili David Correy wa Brazil na rapa Octopizzo wa Kenya.
Katika wimbo huo, Lady Jaydee na Correy wameimba kwa lugha ya Kiingereza huku Octopizzo 'akichana' kwa Kiswahili.
Wimbo huo ulipigwa kwa mara ya kwanza jana jijini Dar es Salaam wakati kampuni ya Coca-Cola ilipozindua promosheni yake mpya ya miezi miwili ya Kombe la FIFA la Dunia 2014 ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi mbalimbali zikiwamo tiketi za kwenda kushuhudia mechi za robo fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Yebeltal Getachew alisema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam huku akizitaja zawadi nyingine kuwa luninga, mipira na fulana.
“Mbali na wateja 14 kupata nafasi ya kwenda Brazil, tutatoa luninga 1,000 za kisasa zenye ukubwa wa inchi 32, mipira 8,000 yenye nembo ya FIFA World Cup na T-shirt 30,000,” alisema Getachew.
Alisema kuwa kupitia Kombe la Dunia, kampuni hiyo itatoa sehemu ya mapato yake kwa jamii inayofanyia biashara.
Alisema washindi watapatikana kwa kunywa vinywaji vya kampuni hiyo na kupata vizibo viwili vinavyotengeneza neno ‘Brazil’ na kimoja cha ushindi ambacho kitakuwa na picha ya kitu ambacho mteja wao atashinda.
Coca-Cola ni mshirika wa FIFA wa muda mrefu tangu 1974. Kampuni hiyo ilianza rasmi kudhamini Kombe la Dunia 1978 na uhusiano wao unatazamiwa kuendelea hadi 2022.
Credit: Bongo Clan
Bravo jidee
ReplyDelete