Habari mpya

WEZESHA WASANII WA NYUMBANI KUINUA KIPATO CHAO,

Inakadiriwa katika ulimwengu kuna watu wanaoongea kiswahili wasiopungua milioni 130. Endapo kati yao  asilimia moja tu (1%) watanunua filamu ya Bongo (Bongo Movie) itapatikana pesa ya Kitanzania shilingi bilioni 6.5 (Tsh 6.5 billion). Na katika hiyo pesa asilimia ishirini tu (20%)akipewa msanii basi atapata kiasi cha sh bilioni 1.3 (Tsh 1.3 billion). 
Je ndugu zangu watanzania tusingekuwa na wasanii matajiri na wenye majina makubwa kama akina Smith au Angelina Jolie? 
Tafakari chukua hatua kwa kununua nakala halisi ya muvi kutoka Tanzania ili kukuza kipato cha wasanii wetu, waweze kuiwakilisha na kuitambulisha vyema Tanzania katika tasnia ya filamu na si filamu tu hata katika muziki kutoka nyumbani.

Idea by: Hon. J. Makamba
Re-written by: Tumsifu Kaoza

No comments