Wateja wa Tigo jijini Mwanza kufikiwa na huduma kwa urahisi baada ya ufunguzi wa duka jipya lililopo katika jengo la Rock City Mall.
|
wageni waalikwa wakifuatilia hotuba kwa makini uzinduzi wa duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza |
Muonekano wa Duka jipya la Tigo Mwenye Jengo la Rock City Jijini Mwanza |
Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika(wa pili kulia) na Msimamizi wa duka la Tigo Rock city Neema Mossama, wakikata keki wakati wa uzinduzi duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza, kushoto ni Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati(wa kwanza kulia) wakishuhudia. |
Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika(kulia) akizungumza na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo(kushoto) Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati, baada ya kuzindua duka la Tigo kwenye jengo la Rock city. |
Mkuu Wilaya ya Ilemela Dk Severine Lalika, akiangalia simu kwenye duka la Tigo kwenye jengo la Rock City jijini Mwanza baada ya kulizindua.
|
Mwanza.Septemba 26, 2019. Kampuni inayoongoza katika maisha ya kidijitali Tanzania,Tigo, leo imefungua duka jipya jijini Mwanza.Duka hilo litawafanya wateja wa kampuni hiyo kupata huduma zote kwa urahisi zaidi ndani ya eneo moja la Rock City Mall.
Duka hilo litatoa huduma zote muhimu kuanzia usajili wa namba za simu kwa alama za vidole, huduma za kifedha ‘Tigo Pesa’ na mauzo ya data na vifaa vya mawasiliano kama simu janja, router na modem kwaajili ya huduma yetu tuliyo zindua hivi majuzi iitwayo ‘Tigo Home internet’.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati amesema hatua ya kufungua duka hilo ni moja ya mkakati wa Tigo wa uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinawafikia wateja kwa wakati nchi nzima.
“Duka hili jipya litampa mteja wetu wasaa wa kutazama na kujaribu bidhaa mbalimbali kabla ya kuamua kufanya manunuzi.Hatua hii imekuja kufuatia maombi ya muda mrefu kutoka kwa wateja wetu waliokuwa wakihitaji uwepo wa duka letu kwenye jengo hili maarufu kibiashara hivyo tumekidhi mahitaji yao,”alisema Madati.
Awali akizindua duka hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Mkoani Mwanza, Dkt.Severine Lalika alipongeza juhudi za Tigo katika kuwekeza rasilimali katika uboreshaji wa huduma na kuhakikisha zinakidhi viwango vya kimataifa.
“Huduma bora kwa wateja ni kitovu cha biashara na zaidi huwafanya wateja wajisikie wanathaminika na kuheshimiwa, Tigo wametekeleza jambo hili kwa vitendo kwa kufanya uwekezaji katika utoaji wa huduma zao jambo linalowapa utofauti wa kipekee sokoni,” alisema Lalika.
Kadhalika,duka hilo linakuwa la nne kufunguliwa mkoani humo huku likiwa na huduma mpya ikiwamo simu zinazotamba kwa sasa aina ya S3 na R7 pamoja na vifaa vya huduma za intaneti kwa makampuni maarufu kama ‘Tigo business’.
Maduka mengine matatu ambayo yanatoa huduma mkoani hapa ni pamoja na Mwanza kiosk-barabara ya Nyerere, Ukerewe shop-Wilaya ya Ukerewe, Sengerema shop-Wilayani Sengerema na Airport kiosk- Uwanja wa ndege wa Mwanza.
//Mwisho//
No comments