|
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie (kulia), akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Sekela Kyomo (kushoto) wakati wa mbio za mbuzi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia jamii zenye uhitaji zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambazo SBL ilikuwa mmoja wa wadhamini kupitia bia yake ya Serengeti Lite. Katikati ni Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa kampuni hiyo John Wanyancha. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa mbio za mbuzi zilizofanyika mwishoni mwa wiki. SBL walikuwa ni moja kati ya wadhamini wa mbio hizo kupitia bia yake ya Serengeti Lite zilizolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye uhitaji. |
|
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya ya Bia ya Serengeti (SBL) wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa mbio za mbuzi zilizofanyika mwishoni mwa wiki. SBL walikuwa ni moja kati ya wadhamini wa mbio hizo kupitia bia yake ya Serengeti Lite zilizolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye uhitaji. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie (wa pili kulia), akiteta jambo na baadhi ya wageni walifika katika viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa mbio za mbuzi zilizofanyika mwishoni mwa wiki ambazo SBL walikuwa ni moja kati ya wadhamini wa mbio hizo kupitia bia yake ya Serengeti Lite zilizolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa kampuni hiyo John Wanyancha. |
|
Baadhi ya wageni waliofika katika vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam wakati wa mbio za mbuzi wakifurahia kinywaji cha Serengeti Lite. SBL walikuwa ni moja kati ya wadhamini wa mbio hizo kupitia bia yake ya Serengeti Lite zilizolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye uhitaji. |
|
Mbuzi wakichuana katika mashindano ya mbio zilizodhamini na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Lite ambazo zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam zikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye uhitaji. |
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie akimfurahia mbuzi mwenye madoadoa ambaye aliibuka mshindi katika mbio za mbuzi zilizoandaliwa kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia jamii zenye uhitaji zilizofanyika katika viwanja vya Farasi vilivyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam. SBL walikuwa ni moja kati ya wadhamini wa mbio hizo. Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Anitha Msangi |
|
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Anitha Msangi akimkabidhi zawadi ya hundi Araf Sykes ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Internet Solution aliyeibuka mshindi baada ya kufanikiwa kubashiri ni mbuzi gani angeshinda katika mbio za mbuzi zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki zikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jamii zenye uhitaji. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie |
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imesema itaendelea kuunga mkono miradi mbali mbali yenye lengo la kutatua kero za jamii na kuleta maendeleoo
Akiongea wakati wa Mbio za Mbuzi kwa mwaka 2018 na ambazo SBL ni mmoja wa wadhamini kupitia bia yake ya Serengeti Lite, Mkurugenzi Mtedaji wa kampuni hiyo Helene Weesie alisema kusaidia jamii ni moja kuchangia maendeleo ya jamii ni moja kati ya vipau mbelele vya kampuni yake
Mbio hizo zilizoandaliwa na Klabu ya Rotary ya Oysterbay Dar es Salaam zilikuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia miradi ya kimaendeleo kama upatikanaji wa maji safi, elimu na mingineyo.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, udhamini wa mbio hizo ni mwendelezo wa mambo ambayo kampuni hiyo imekuwa ikisaidia ili kuboresha maisha ya jamii haswa zile zenye uhitaji Zaidi katika sehemu mbali mbali nchini.
“SBL pia imekuwa ikisaidia jamii zinazoishi katika sehemu kame na zisizo na huduma ya maji safi na salama. Mpaka kufikia hivi sasa, zaidi ya watu milioni moja sehemu mbali mbali nchini wameweza kunufaika na visima ambavyo SBL imevichimba,” alieleza
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma John Wanyancha alisema SBL inaendesha mradi wa kuwasaidia wakulima kuzalisha zaidi mazao ambayo hutumika kama malighafi katika uzalishaji wake wa bia ikiwamo shayiri, mtama, ulezi na mahindi.
Mradi huo unaojulikana kama Kilimo-biashara unatekelezwa katika mikoa ya Arusha, Manyara, Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Morogoro, Shinyanga na Dodoma.
Kwa mujibu wa Wanyancha, mradi wa Kilimo-Biashara umetoa jibu kwa tatizo la ukosefu wa masoko kwa wakulima wa ndani ambao kipindi kirefu wamekuwa wakilia kutokana na ukosefu wa soko la uhakika la bidhaa zao.
“Hii ni fursa pekee ambayo watanzania wanahitaji kuitumia na hasa ikizingatiwa kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha soko la ndani. Serengeti inaamini kuwa watanzania wana uwezo wa kuzalisha malighafi bora na tukazitumia kutengeneza bidhaa bora,” alisema
Chini ya mradi huo Wanyancha alisema SBL inatoa mbegu zenye ubora bure kwa wakulima na pia kuwaunganisha na taasisi mbalimbali za kifedha ili kupata mtaji utakaohitajika kwa kilimo cha mashamba makubwa.
MWISHO.......
No comments