SBL yazindua bia mpya iitwayo Serengeti Premium Lite
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akiwakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi amezinduwa bia mpya ya Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), inayojulikana kama 'Serengeti Premium Lite'.
Akisoma hotuba ya Waziri Mwakyembe katika uzinduzi huo, Bi. Kihimbi alisema wizara inaipongeza kampuni ya SBL kwa kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania yaani jina la Hifadhi ya Taifa Serengeti kupitia bia yao. Alisema Bia mpya ya Serengeti Premium Lite iliyopikwa kisasa iliyozinduliwa na SBL inaendelea kulitangaza hifadhi ya Serengeti hivyo kuwataka wananchi wapenzi wa kinywaji hicho kuitumia ili kutangaza nchi.
“Programu za jamii zinazoendeshwa na SBL katika sekta ya elimu, kilimo na ujasiriamali zimewezesha vijiji vingi hapa nchini kupata maji safi, watoto kupata elimu ya juu na mamia ya wakulima kupata masoko kwa ajili ya kuuza mazao yao ambapo SBL hununua mazao yao kama malighafi inayotumika kuzalishia bia,” alisema Mwakyembe.
Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta alisema SBL, ikiwa ni mojawapo ya kampuni kubwa zinazozalisha bia hapa nchini, imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa ni muendelezo wa bia mama ya Serengeti Premium Lager iliyoko sokoni kwa zaidi ya miaka 20.
“Bia ya Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa namna ya kipekee kwa kutumia utaalamu wa kisasa wa uzalishaji bia. Ina ladha kamili inayoburudisha zaidi ya bia za aina ya lite ambazo kwa sasa huuzwa reja reja sokoni,” alisema Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa kwa Sh.1,500 kwa chupa na kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuia ya wanywaji wake
ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitafuta bia halisi ya Kitanzania. “Pamoja na kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa biaya Serengeti Premium Lite, niseme kuwa ni bia halisi ya kitanzania yenye kiburudisho na ladha nyepesi.
ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitafuta bia halisi ya Kitanzania. “Pamoja na kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa biaya Serengeti Premium Lite, niseme kuwa ni bia halisi ya kitanzania yenye kiburudisho na ladha nyepesi.
Huu ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii kwa muda mrefu. Tuna amini kuwa bia hii ya Serengeti Premium Lite, ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishaji bia (bremasters) wa kitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri watakapo kuwa wakifurahia urithi wetu wa aina hii ya bia”, alisema Mehta.
Aliongeza kuwa, “Bia ya Serengeti Premium Lite ina ubora ule ule wa kimataifa sawa na bia mama ya Serengeti Premium Lager ambayoimepokea zaidi ya medali 10 za ubora wa kitaifa na kimataifa.”
No comments