Habari mpya

Bia ya Serengeti yasherehekea kutimiza miaka 20



 Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari  ambapo alitangaza maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996. Anayefuatia ni Meneja masoko wa SBL  Anitha Msangi na kulia  mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka  .Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam

Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996.Anayefuatia katikati ni Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi na mwishoni kulia ni Mkurungezi mkuu wa SBL  Helene Weesie.Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.

Mpishi Mkuu mtanzania  Winston Kagusa aliyefanikiwa kuchanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchini kupata  kinywaji hiki  cha Serengeti Premium Lager kinachopendwa na wengi.


 Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akiongoza katika kuzindua chapa mpya ya Serengeti Premium Lager sherehe ambazo zinaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya bia hiyo kulia kwake ni Meneja Masoko wa SBL Anitha na kushoto kwake wa kwanza ni Mpishi Mkuu wa kwanza wa Serengeti Premium Lager Winston kagusa na mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko  Cesear Mloka.Hafla hii ilifanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL John Wanyacha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa waandishi wa habari ambapo Bia ya serengeti premium lager inatimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake na pia kuzinduliwa kwa chapa yenye muonekano mpya.Mkutano huu ulifanyika mapema leo katika hotel ya Hyatt Regency
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema leo

  • SBL yaizindua bia hiyo katika muonekano mpya

  • Yashinda zaidi ya medali 10 za ubora wa kimataifa

Dar es Salaam  Oktoba 27, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo  imetangaza kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.

Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, amesema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja  wake na umma wa Watanzania  kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.

 “Tunawashukuru  wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na wadau wote  ambao kimsingi wametusaidia  na kuwa nasi  katika safari yetu hii ya mafaniko,” amesema Weesie.

Bia ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa  ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.

Aidha Mkurugenzi huyo ameendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.

“Tunaona fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager  katika  ubora uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi kutokana na kutambuliwa  na wateja wetu wa ndani  pamoja na medali  zaidi ya 10  za kutambulika kimataifa  ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium Lager  katika ubora wa hali ya juu  kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” amesema Weesie.

Uzinduzi wa muonekano mpya wa  bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.


No comments