Mh. Deo Ngalawa atoa msaada wa vifaa vya michezo Wilayani Ludewa
Katika kusaidia na kuendeleza michezo wilayani Ludewa Mh. Deo Ngalawa amejitolea jezi kwa kila kijiji katika Wilaya ya Ludewa ambapo kufuatia mpango huo vijiji 77 vimenufaika. Hiyo imefuatia kudorora kwa michezo katika Wilaya ya Ludewa kutokana na hali duni na mwamko mdogo wa michezo kitu kinachopelekea kukosekana kwa wadhamini si katika mchezo wa mpira wa miguu bali hata katika michezo mingine na sanaa kwa ujumla.
Pamoja na hilo Mh. Mbunge ametoa vifaa vya michezo kwa timu 8 za mpira wa miguu zilizoshiriki ligi ya walaya Wilayani Ludewa mjini.
Akitoa vifaa hivyo Mh. Ngalawa alisema kuwa timu hizo ni mfano tu lakini tayari ameshaandaa jezi za kila kijiji kwa vijiji (77), ambapo yatafanyika mashindano kwa kila Kata na baadae kwa kila tarafa na hatimaye Wilaya ili kumpata mshindi wa Wilaya ya Ludewa. Licha ya mashindano hayo ya mpira wa miguu pia yatafuata mashindano ya vikundi vya ngoma za Utamaduni na vikundi vya wasanii mbalimbali ili kuinua vipaji vya wanaludewa. Alisema kuwa Wilaya ya Ludewa kuna vipaji vingi lakini vinatakiwa kuibuliwa na tayari yeye kama mbunge ameliona hilo na tayari ameshaanza kulifanyia kazi.
Diwani viti maalumu tarafa ya Liganga, Selina Haule akipokea Jezi kwa niaba ya Diwani wa Kata ya Mundindi. Kulia ni katibu wa Ludifa, Stephano Mahundi na kushoto ni katibu Jerome Bange.


Post Comment
No comments