Habari mpya

Mbunge wa wilaya ya Ludewa asaidia taasisi za kidini

Katika jitihada za kusaidia wananchi wake na kuhakikisha wanapata mahali pazuri pa kuabudia Mh. Mbunge amekuwa akisaidia taasisi mbalimbali za dini. Hii imekuwa ni jadi kwa wabunge wa wilaya ya Ludewa kwani hata mbunge aliyepita Ndugu Filikunjombe (Astarehe kwa amani) alikuwa na utamaduni huo kwa wananchi wake.
Katika jitihada hizo Mh. Deo Ngalawa katika ziara yake ya mwishoni mwa mwezi jana ameahidi kuchangia Kanisa la Anglikana katika kijiji cha Mavanga mifuko ya saruji 450 yenye thamani ya Tsh. 8,750,000 na tayari ameshatoa kiasi cha Tsh. 2,000,000 kwa ajili ya zoezi hilo la ujenzi wa kanisa.


No comments