Habari mpya

Shehena ya sukari tani 4579.2 zakutwa kwenye maghala Mbagala


May 06 2016 Rais Magufuli alizungumza na wawananchi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kwenda Arusha. Rais Magufuli alitoa maagizo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali.

Sasa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa  kuwa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya suala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi. 

TAKUKURU ilitembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo haya ndio waliyoyabaini…..

TAKUKURU imebaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari hiyo ili iweze kusambazwa

Katika eneo la Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.

Kumekuwepo na mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.

Source. Jestina-George Blog

No comments