Nimpe nini mama'ngu?
Alinilea mapema,kabla ya kuona jua,
Ninamheshimu mama,kweli nimemsumbua,
Hadi leo nasimama,na kuongea najua,
Mama nitakuheshimu,umefanya mengi kwangu.
Ninamheshimu mama,kweli nimemsumbua,
Hadi leo nasimama,na kuongea najua,
Mama nitakuheshimu,umefanya mengi kwangu.
Usiku haukulala,mie waniangalia,
Waja kujua hujala,wengine wamesinzia,
Mie nikigalagala,shuka lako nafunua,
Mama ninakushukuru,sijui nikupe nini.
Waja kujua hujala,wengine wamesinzia,
Mie nikigalagala,shuka lako nafunua,
Mama ninakushukuru,sijui nikupe nini.
Mama wewe unapika,mie kukaa sipendi,
Mama yangu umechoka,mie kulia hupendi,
Mama umeshughulika,mama wewe ni mshindi,
Mama wewe ni shujaa,mola anakutambua.
Mama yangu umechoka,mie kulia hupendi,
Mama umeshughulika,mama wewe ni mshindi,
Mama wewe ni shujaa,mola anakutambua.
Baba karudi usiku,wewe wamfungulia,
Kanywa pombe wamshuku,ila hujamnunia,
Huko amekula kuku,wengine kanunulia,
Mama umevumilia,ushindi utakujia.
Kanywa pombe wamshuku,ila hujamnunia,
Huko amekula kuku,wengine kanunulia,
Mama umevumilia,ushindi utakujia.
Leo baba hanywi pombe,na pia akusifia,
Kimwona ana kikombe,maziwa anajinywea,
Kikumbuka usiombe,baba yangu atalia,
Mama nikulipe nini,ishi nami siku zote.
Kimwona ana kikombe,maziwa anajinywea,
Kikumbuka usiombe,baba yangu atalia,
Mama nikulipe nini,ishi nami siku zote.
Mama unachechemea,ulipigwa wanambia,
Kweli sikutegemea,mama unavumilia,
Mungu wamtegemea,muumba waniambia,
Mama umebarikiwa,mbinguni tapokelewa.
Kweli sikutegemea,mama unavumilia,
Mungu wamtegemea,muumba waniambia,
Mama umebarikiwa,mbinguni tapokelewa.
Si kwamba nakusifia,baba nimemchukia,
Yeye pia kanilea,siwezi kumchukia,
Heshima nampatia,yeye anihudumia,
Mama yangu nakupenda,wewe ni shujaa wangu.
Yeye pia kanilea,siwezi kumchukia,
Heshima nampatia,yeye anihudumia,
Mama yangu nakupenda,wewe ni shujaa wangu.
Mama mungu akulinde,wewe umebarikiwa,
Matatizo uyashinde,mjukuu waletewa,
Pia baba umpende,mama utabarikiwa,
Mama yangu wewe bora,utabaki kuwa bora..
Matatizo uyashinde,mjukuu waletewa,
Pia baba umpende,mama utabarikiwa,
Mama yangu wewe bora,utabaki kuwa bora..
No comments