Habari mpya

Mechi ya kati ya Yanga na Ndanda kufanyika uwanja wa taifa Dar es salaam.

Mpaka sasa taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Ndanda na Young Africans umepangwa kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mara baada ya Yanga kuomba hivyo na Ndanda kama timu mwenyeji kuridhia kuuhamisha kutoka Nangwanda Sijaona wa Mtwara.
Kwa nyakati tofauti, mwishoni mwa wiki iliyopita Young Africans ilituma maombi kwa Ndanda kadhalika TPLB kuomba ridhaa ya mchezo huo kufanyika Dar es Salaam kwa kuwa inatarajiwa kusafiri Jumapili alfajili kwenda Angola kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidia ya Sagrada Esperanca ya Angola.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TPLB, Ndanda imekubali ombi la Young Africans iliyoomba mchezo huo uhamishwe kwa malengo ya kuisaidia Young Africans kuwahi usafiri ndege kwenda Angola ambako wanatarajiwa kucheza na wapinzani wao ama Mei 17 au 18, mwaka huu.

No comments