Habari mpya

Juma Kaseja, tajiri anayekipiga na Mbeya City Fc (Sehemu ya tatu)

Na;Mwanakalamu
Kwanza napenda nikuombe radhi mpenzi msomaji wa makala hii kumuhusu Tanzania One Juma Kaseja kwa kushindwa kuwa nanyi kwa siku mbili mfululizo.Palikuwa na tatizo la kiufundi hivyo nikashidwa kuwaletea uhondo.Katika sehemu iliyopita tuliishia pale nilipokuwa na Kaseja mdogo kule ziwani tumekaa mchangani,Tuendelee.
Baada ya kukaa pale mchangani tukiangalia mazingira ya pale ufukweni kwa muda huku kila mtu akiwa na lake kichwani mwake , nikapata cha kuongea.
''Hivi kama nataka kuoga nitaenda kuoga wapi wakati pana watu kibao?''
''Hapa wamegawa kwa wavulana na wasichana, unaona wale akina mama? pale wanaoga wanawake na hapa tulipo ni sehemu ya kuoga wanaume , wamegawa hivi hivi ufukwe mzima''Alieleza Kaseja mdogo.
''Sawa , ila mbona hapa kuna wakawake pia?''Niliuliza.
''Hapa pana wasichana pia kwa kuwa wavuvi wanakuja na samaki hivyo huja kununua samaki pia hata kama mtu atataka kuoga anakuwa amevaa bukta''Hapo nikafungua tena akili huku nikijiuliza kama nitaweza kuoga ziwani kwa muda wote nitakao kuwa pale kijini.
''Sawa nimekuelewa Kaseja wangu, kwa hiyo huwa unakuja kufanya mazoezi ya kudaka huku?''
'' Mie nadaka pale uwanjani huku kwenye mchanga watu waoga ndo hujifunzia huku mie najifunzia kwenye jamvi la uwanja wa taifa''Anajigamba  mtoto.
''Kwa hiyo uwanja wenu una kapeti/jamvi kabisa?'' Nauliza kinafiki lakini kabla ya kunijibu anainuka na kukimbilia mahali ambapop wengi wanakimbilia, kumbe wavuvi wamekuja kutoka kuvua watu wnakimbilia mgao naona kundi kubwa la watu wameshika mtumbwi ambao nilihisi ulihitaji watu wanne tuu kuuweka ufukweni.
Baada ya dakika kama kumi hivi Kaseja mdogo anakuja na samaki mkononi na ananishawishi tuelekee nyumbani akanitengenezee samaki wale nile.
Tukiwa njiani Kaseja mdogo ananieleza mambo mengi juu ya watoto wenzake wanaopenda kudaka na wanajiita Kaseja ila anaamini hakuna wa kumfikia yeye ambaye ni mrithi halisi wa Kaseja Tanzania one.
Namtazama usoni kumsoma bila mwenyewe kugundua , anaonekana kuwa makini na alichokuwa anakiongea , aliamini alichokisema ambacho bila shaka yoyote kilitoka moyoni mwake maana alikisema kwa ari kubwa sana.
Moyo wangu ukaumia baada ya kufikiria kama ataingia kwenye kundi la watoto na vijana wengi waliojaribu kuwa kama Kaseja katoka kila mkoa nchini, kila wilaya, kila kata, kila kijiji ama hata mtaa ni mamia ya watoto lakini wanishia kudaka kwenye mabonanza yanayoandaliwa na wanasiasa  karibu na kipindi cha uchaguzi.Ni mamia ya watoto lakini wengi wanaishia kuwa maarufu mitaani mwao umaarufu unaopelekea kupewa ofa za pombe ama wanawake pale wanapofanikiwa kudaka vyema.
Lakini nilimfikiria tena Kaseja Tanzania one anayedakia Mbeya City, ana historia yenye mikasa mingi ambayo kwa mpenda soka halisi lazima umuumize.Kaseja ambaye amewafanya wengi kupenda kudaka, amewafanya wengi kufuatilia soka, Kaseja aliyewafanya hata wasichana ambao soka si kitu wanachokipenda lakini wakajikuta wakipenda soka ili tuu kumtazama, Kasejahalisi ambaye amefanya maelfu ya watu kuishabikia klabu ya Simba , Kaseja aliyewaliza watu wa simba pale alipohamia Yanga lakini alifanikiwa kupewa heshima ya mashabiki hata alipokuwa upande wa pili.Kaseja ambaye hata watoto wasiowahi kumwona wanaliimba jina lake,Kaseja golikipa ambaye anaingia kwenye rekodi za kuwa  katika kundi dogo la wachezaji waliodumu kwenye soka kwenye kipindi kirefu.
Ndiyo Kaseja aliyetemwa na Simba kienyeji licha ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka saba, ndiyo ni huyo huyo huyo ambaye leo hii kuna viongozi wa soka wanatamani wapenda soka tumsahau kwa nguvu , tuusahau na mchango wake kwenye soka la Bongo ama Afrika mashariki kwa Ujumla kwa kuwa tuu  hajawai kuleta tunzo ya uchezaji bora Afrika ndiyo ni huyo ambaye leo hii kuna mtoto ambaye anatamani kuwa kama yeye licha ya kutomwona.
Tunafika nyumbani hapo nakutana na taarifa inayonitaka niondoke siku inayofuata kurudi jijini Dar es salaam , taarifa ambayo inamfanya hata Kaseja mdogo asikitike.
Lakini namwahidi kitu ambacho kinamfanya arukeruke kwa furaha.
Ni kitu kani hicho?
TUKUTANE KESHO AMBAPO TUTAMALIZIA SIMULIZI HII YA KASEJA NA KUNZA NYINGINE ITAKAYOMUHUSU AMIS TAMBWE.

No comments