Chura ya Snura afungiwa mazima Tanzania
Snura afungiwa kujihusisha na Sanaa Tanzania. Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.
Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini.
Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar mapema asubuhi ya leo. Amedai kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.
Muda kama wa lisaa limoja lililopita Mtandao wa Kalamu Yangu umeinasa habari hiyo ikipamba vichwa kadhaa vya Blog hapa Bongo na kuwa mada ndani ya mitandao ya kijamii.
No comments