Mh. Mwigulu Nchemba awataka waliosababisha maafa kukamatwa mara moja na kupelekwa kunakohusika

Kufuatia
migogoro ya ardhi inayoendelea sehemu mbalimbali hapa nchini hasa baina
ya wafugaji na wakulima na ile ya wananchi na wawekezaji imemlazimu Mh.
Mwigulu Nchemba kufika Mkoani Morogoro wilaya ya Mvomero ambako
yalitokea maafa kufuatia vurugu baina ya wakulima na wafugaji. Nchemba
amelaani vikali maafa hayo na kutoa rai ya wahusika waliotekeleza unyama
huo kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakani na kuwaasa wananchi
kuacha kujichukulia hatua mkonini.
Pia
amesema zitaundwa kamati kwa kila kijiji kwa pande zote mbili
ilizoingia katika mgogoro ili kubaini ni nani hasa mvamizi wa eneo la
mwenzakeili hatua iweze chukua mkondo wake.
Pia
amemuagiza mkuu wa wilaya ya Mvemoro kuhakikisha watu waliojeruhiwa,
wanapatiwa matibabu kwanza bila kuchelewa na hatua za kisheria kwa wenye
hatia zifuate.
Endela kufuatilia Mwanaharakati Mzalendo Media kwa taarifa zaidi.

No comments