Habari mpya

Watangaza nia kuwania kiti cha Ubunge kilichoachwa na Marehemu Deo Filikunjombe waendelea kuchukua fomu akiwemo mdogowake marehemu na Msanii Masanja Mkandamizaji

Masanja Mkandamizaji
MSANII maarufu na mwigizaji Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la (Masanja mkandamizaji) ameahidi kuvaa viatu vya Deo H. Filikunjombe kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Ludewa na kusema ana uwezo mkubwa na kasi kama ya marehemu Filikunjombe ambaye alikuwa rafiki yake.
Ameyasema hayo alipokuja kuchukua fomu ya kugombea kupata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi,jumla ya watu tisa akiwemo mdogo wa marehemu Fillipo Filikunjombe ambaye ni mwanasheria wa TCRA wamechukua fomu ili kuweza kuomba ridhaa. Wengine waliochukua fomu ni pamoja na James Mgaya, DEo Ngalawa, Simoni Ngatunga, Eng. Chaula, Mstaafu Mpangala na Johnson Mgimba.

No comments