Mrithi wa Deo Filikunjombe apatikana, Masanja awa msindikizaji
Jimbo la Ludewa ni moja
kati ya majimbo ambayo wananchi wake hawakuweza kupiga kura kumchagua
mbunge wao katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 2015
kutokana na mmoja wa wagombea kupitia Chama cha Mapunduzi kufariki dunia
baada ya kupata ajari ya chopa.
Kwa
muda kidogo Wanaludewa wamekuwa wakitafakari ni nani kuwa mrithi wa
kipenzi chao Deo na siku za hivi karirubuni wameweza kujitokeza watia
nia kadhaa kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya chama cha Mapinduzi
akiwemo mdogo wa marehemu Deo, Filipo Filikunjombe, Eng. Chaula, Mstaafu
Mpangala, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji), Deo Ngalawa na
wengine.
Siku
ya jana ndiyo ilikuwa siku ya kufunga kazi ndani ya chama cha Mapinduzi
ili kumpata mtu mmoja atakayekiwakilisha chama hicho. Baada ya masaa
kadhaa ya upigaji kura na uhesabuji wa kura uliofanywa na wagombea
wenyewe (kama tulivyopata taarifa kutoka chanzo kimoja mtandaoni) ndipo
matokeo yakawa kama ifuatavyo:
- Deo Ngalawa 537
- Philipo Philikunjombe 501
- Mpangala 03
- Emmanuel Masanja 19
- James Mgaya 72
- Evaristo Mtitu 21
- Chaula 38
- Na zilizoharibika ni 2
Kwahiyo kwa matokeo hayo yanamuwezesha bwana Deo Ngalawa kuwa mgombea wa kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM.
Mwisho wa safari moja ndio mwanzo wa safari nyingine, ya kuelekea Bungeni.
Post Comment
No comments