Baadhi ya picha za matukio katika safari ya kumsindikiza Mpendwa wetu Mh. Deo Filikunjombe, Egdi Nkwera na Casablanca Haule Ludewa Mjini
Lazaro Nyarandu
Zito Zubery Kabwe akiweka taji la maua katika kaburi la Rafiki yake mpendwa Deo Filikunjombe, leo jioni
SPIKA
wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda amesema kuwa Mbunge
marehemu Deo Filikunjombe, alikuwa ni mbunge wa tofauti kutokana na
alivyo kuwa akifanya kazi zake na alikuwa hakai bungeni alikuwa anapenda
kukaa na wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Spika
Makinda alisema kuwa Filikunjombe alikuwa ni mbunge wa tofauti na
alipenda kuwa na wananchi mda wote na kila alipokuwa akimaliza bunge
alikuwa anakimbilia kwa wananchi wake.
Alisema kuwa alikuwa ni mpiganaji kwa
kufanya kile anacho kiamini serikali inaenda tofauti hukipigia kelele na
huhakikisha wananchi wanapata haki zao.
Alisema kuwa wananchi wamempoteza
mpigania haki zao na wahakikishe kuwa wanaangalia mbunge atakeye kuwa
tayari kumalizia mipango yao aliyo kuwa ameianza mbunge wao.
"Filikunjombe alikuwa ni mbunge jasiri
na alikuwa akiwatetea WanlLudewa na Watanzania kwa ujumla.
Aliongeza kwa kutoa wito wa watu wanao
litaka jimbo la Ludewa kuhakikisha kuwa wanakuja kutekeleza yale aliyo
kuwa ameyaanza Deo na kukamilisha mipango yake huku akisema kuwa mbunge
huyo alikuwa na mipango ya miaka mingi kuifanya Ludewa ya tofauti.
Alisema kuwa Deo alikuwa ni mbunge mwenye
kupenda maendeleo na kuleta umeme katika jimbo hilo pamoja na barabara
za kufika katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Aidha wa upande wake Rafiki yake mpendwa
Wa Filikunjombe, Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zito Kabwe
amesema kuwa anasikitika kutokea kwa msiba wa rafiki yake mpendwa na
kuwa hatoweza kumpata rafiki wa aina ya Filikunjombe kutokana na alivyokuwa.
Alisema kuwa kwa wakazi wa Ludewa
wamempoteza mtu muhimu sana na kuwa hawata kuja kumpata mbunge kama huyo
licha ya kuwa watapata mbunge lakini kufanana na Deo ni vigumu.
Aliongeza kuwa Deo kwakuwa aliwapenda Wanaludewa wakati ajali inatokea alijaribu kuruka na mwili wake
ulikutwa mbali kidogo na mabaki ya ndeke inaonekana alikuwa anataka
kujiokoa na kuungua na moto uliokuwa ukiwaka kutoka ilipo angukia Ndege.
Akihubiri katika ibada ya mwisho ya
msiba wa marehemu hao watatu ambao ibada ilikuwa ni moja Askofi wa
Kanisa la Romani Katoliki jimbo la Njombe, Ask. Alfred Maluma alisema
kuwa msiba huo ni mkubwa kwa kuwa umehusisha watu watatu wanao tokea
sehemu moja na kuwatia moyo wafiwa kwa kuwaambia kuwa wawe wavumilivu
katika siku hizi ngumu kutokana na msiba wenyewe ulivyotokea na ughafla
wake.
Akielezea safari ya kuja kutoka Mjini
Njombe kuelekea wilayani Ludewa alisema kuwa walikuwa wakisimamishwa
kila mahali na wananchi wakilia kuonyesha masikitiko yao juu ya kifi ya
Filikunjombe.
Alisema kifo chake kimewashitua wengi
kutokana na alivyo kuwa akiwasaidia wananchi na kuwa wananchi katika
vijiji mbalimbali walikuwa wakilia kwa sauti licha ya kupita Usiku
katika maeneo hayo.
Mwili wa marehemu uliwasili usiku majira
ya saa 7 usiku katika mji wa Njombe baada ya kufanya ibada katika kanisa
katiliki Njombe mjini na kuanza safari kuingia nyumbani kwao Mjini Ludewa. Ibada ya kuwaaga Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake Egid Nkwera,
Casablanka Haule ambao walikuwa wakisafiri kwa pamoja kutoka jijini Dar
Es salaam kuja mkoani Njombe ilifanyika leo siku ya jumapili na kumalizikia katika makaburi ya Ludewa Mjini.
Msiba huo ambao umekuwa mkubwa kwa
wakazi wa Jimbo la Ludewa ulio kusanya umati mkubwa wa wakazi wa Ludewa
na watu kutoka sehemu mbalimbali maduka katika mji wa Ludewa yalifungwa
kwa siku mzima huku wakazi wa mji huo wakiomboleza msiba wa mbunge wao.
Katika msiba huo kuna viongozi
mbalimbali waliofika kuomboleza akiwemo Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr.
Rehema Nchimbi, Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu, Wiliamu
Lukuvi, na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi wa nyadhifa
mbalimbali.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi
wa Wilayani Ludewa wamesema kuwa hawatampata mmbunge mweye aina ya
mbunge wao na kuwa Msiba huo umetokea kwa ghafla wamesikitika
sana ni bora angeumwa wangejua anaumwa.
Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe
Deo Sanga na mgombea wa ubunge jimbo la Makambako alisema kuwa Jumapili
iliyopita alikuwa katika jimbo hilo kupiga kampeni kumsaidia marehemu
anasikitika kutokea kwa msiba huo, huku akibubujikwa na machozi alisema
kuwa alipiga kampeni katika vituo saba na kuwa aliagwa na mgombea huyo
jumanne iliyopita alimuaga kuwa anaenda Dar es Salaam.
WASTAREHE KWA AMANI NDUGU ZETU WAPENDWA, MBELE YETU NYUMA YAO,
AMEN.

No comments