WANENGUAJI WAWILI WAFUNGWA JELA MISRI
Mnenguaji kiuno
Mahakama nchini Misri imewahukumu wanenguaji viuno wawili
kufungwa jela miezi sita kila mmoja kwa kuchochea uasherati.
Suha Mohammed Ali na Dalia Kamal Youssef, wanaojulikana
kama Shakira na Bardis wa Misri, walikamatwa kwa kusakata ngoma katika video
wakiwa nusu uchi.
Mawakili waliwasilisha malalamishi kortini, wakisema
wawili hao walikuwa kero kwa umma kimaadili na waliwaharibia sifa wanawake wa
Misri.
Mwezi Machi, mchezaji densi mwingine kwa jina Safinaz
alifungwa jela miezi sita kwa kuikosea heshima bendera ya taifa hilo.
Alikuwa ametokea kwenye video akivalia nguo yenye rangi
za bendera ya Misri.
Msakataji densi mwingine, Salma el-Fouly, alifungwa miezi
sita mwezi Julai kwa kucheza kwenye video akiwa amevalia mavazi mafupi na
kuonekana kuchezea waume.
Mwanamume aliyepiga picha hizo za video pia alifungwa jela miezi sita, huku mwanamume wa pili aliyetokea kwenye video hiyo na ambaye pia alihudumu kama produsa akihukumiwa mwaka mmoja jela bila yeye kuwa kortini.


No comments