Breaking News: Kamati kuu CCM yaagiza kura za maoni kurudiwa katika majimbo matano
\
Nape Nnauye akizungumza kwenye moja ya mikutano na waandishi wa habari
KAMATI
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CC) imeagiza kurudiwa kwa
uchaguzi katika majimbo matano kutokana na dosari mbalimbali
zilizojitokeza katika mchakato wa kura ya maoni.
Majimbo hayo ni Makete,Busega,Ukonga,Rufiji na Kilolo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mjini Dodoma Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Ndugu Nape Nnauye amesema mchakato huo utarudiwa siku ya alhamisi
Agosti 13.
Amesema baada ya uchaguzi huo matokeo yatapelekwa katika vikao vinavyoendelea kwa ajili ya uamuzi.
Akizungumzia kuhusu vikao vinavyoendelea Ndugu Nape amesema
vikao hivyo vinaendelea vizuri ambapo jana kikao cha kamati ya maadili
kiliendelea mpaka usiku.
Amesema leo wanatarajia kumaliza kikao cha CC ambapo kesho na
kesho kutwa watamaliza na kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho(NEC)
kama ilivyopangwa.


No comments