MASOUD KIPANYA AIGOPA SIASA YA BONGO LICHA YA KUSHAWISHIWA KUINGIA KATIKA SIASA
Mchora katuni mashuhuri Masoud Ally Kipanya alimaarugu kama Kipanya amefunguka na kusema kuwa amekuwa akishawishiwa nawatu
wengi sana kuingia katika siasa na kufanya siasa kutokana na harakati
zake za kuikosoa Serikali na viongozi kupitia sanaa yake ya uchoraji,
Masoud alisema hayo alipokuwa akichat Live Kikaangoni Live kupitia
ukurasa wa facebook wa EATV.
Moja
ya shabiki alitaka kujua kama Mchoraji huyo anaweza kuingia katika na
kugombea nafasi ya Ubunge ili aweze kuwakilisha wananchi mbungeni na
kuweza kufikisha mawazo yake ambayo huwa anayafanya katika kurekebisha
au kukumbusha Serikali pamoja na viongozi mbalimbali kupitia sanaa yake
ya uchoraji wa katuni.
"Kwa
sasa sijajua bado ,ingawa nashawishiwa na watu lakini bado naiogopa
siasa, sijaamu ingawa bado ila naamini naweza kuwasaidia watanzania bila
ya kuwa mbunge, diwani au rais. kupitia hizi hizi fani zetu za sanaa "
Mbali
na hilo Masoud Kipanya alisema kupitia sanaa yake ya uchoraji ni moja
ya kitu ambacho kwa sasa kinamuingizia pesa nyingi kuliko kiyu kingine
chochote akifanyacho na kudai kuwa sanaa hiyo hiyo imeweza kumpa nafasi
ya kufahamiana na watu na pia imempa nafasi ya kuifahamu dunia, ingawa
anakiri wazi kupitia kazi yake hiyo ya uchoraji muda mwingine huwa
anapata vitisho kutoka kwa viongozi ambao wanakuwa wamechorwa na
kutafsiri tofauti kile alichokichora na kudai kuwa changamoto hiyo
inakwenda mpaka kwa wahariri kwani kuna muda wanaogopa kuchapisha baadhi
ya katuni zake.
"Sanaa
imenipeleka sehemu kubwa sana ya dunia. imenipa heshima kubwa sana,
lakini pia inanilipa sana. pato langu kubwa linatoka kwenye uchoraji
sema napata changamoto na kubwa ni pale wanaochorwa wanapokasirika na
wakati mwingine kusababisha matatizo hata ya vitisho. lakini changamoto
nyingine ni wahariri wa magazeti ninayofanyia kazi kuziogopa baadhi ya
katuni na kutozichapisha"
"vitisho
viko vingi sana. sana kabisa, bahati nzuri wanasiasa wengi wameingia
katika siasa wamenikuta ninachora katuni, hiyo imesaidia sana kuwafanya
wengi wao waniheshimu na wakati mwingine hata kuogopa." Aliongeza Masoud
Kipanya
MAISHA PLUS
Maisha
ni kipindi cha Televisheni ambacho huwa kinafanyika mwaka lakini kwa
mwaka huu Masoud Kipanya ameonyesha wasiwasi kwa kipindi hicho huenda
kisiweze kufanyika kutokana na upungufu wa pesa kwa ajili ya kuendesha
kipindi hicho lakini pia aliweza kuweka wazi faidi kubwa yeye aipatayo
katika kuendesha kipindi hicho ni kuona analeta mabadiliko ya kujitambua
kwa vijana.
"Maisha
Plus inafanyika kila mwaka lakini mwaka huu tunaweza tusiifanye
kutokana na changamoto za kifedha, maisha plus huwa inagharimu pesa
nyingi sana na moja ya faida ya kwanza kubwa na muhimu kwangu mimi
katika kipindi cha Maisha Plus ni kuona nasaidia kuleta mabadiliko ya
kujitambua kwa vijana."
Hivyo
naweza kusema Maisha plus ipo, mwaka huu tunaweza tusiifanye ingawa
bado tuko kwenye mazungumzo na wadhamini wetu ambao tumefanya nao kwa
miaka miwili mfululizo, wanataka tupunguze bajeti na sisi tunaogopa
kupunguza kwa sababu gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa sana"
Lakini
mbali na hilo Masoud Kipanya aliweza kuelezea kwanini imekuwa ni ngumu
sanaa kwa baadhi ya washiriki na washindi wa matamasha mbalimbali ya
kuonyesha vipaji na kusema kuwa imekuwa ni ngumu sana kwa waandaaji wa
matamasha hayo kuwafuatilia washiriki na washindi baada ya muda wao
kupita na kusema kuwa muda mwingine familia zinakuwa zinawawekea ukuta
waandaaji hao kwa kuhisi kwamba watatumia hizo pesa wanazokuwa
wameshinda watu hao jambo ambalo linafanya watu washindwe kuwafanyia
mipango watu hao maana wanakuwa mbali nao.
"
Kwa hapa nyumbani hatuna mfumo mzuri wa ufuatiliaji hasa baada ya
mashindano kumalizika, nikiwa kama muaandaaji, hiyo ni changamoto kwetu.
lakini pia mara nyingi mtu akishinda, famili huwa haipendi aingiliwe
katika mipango yake wakiamini pengine mtaitolea macho zawadi aliyopata
jambo ambalo linaleta umbali mkubwa kati ya muaandaaji na mshindi"
credits:eatv
MASOUD KIPANYA AIGOPA SIASA YA BONGO LICHA YA KUSHAWISHIWA KUINGIA KATIKA SIASA
Reviewed by Unknown
on
10:53 PM
Rating: 5
Reviewed by Unknown
on
10:53 PM
Rating: 5


No comments