Habari mpya

MH. MWIGULU NCHEMBA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KUPITIA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERA YA TUMAINI LA WATANZANIA 2015


Sasa  ni  zamu  ya  Mwigulu  Nchemba  kutangaza  nia kama ilivyofanyika katika Ukumbi wa Mwl. Nyerere katika chuo cha mipango Dodoma kwa  tiketi  ya  Chama  cha  Mapinduzi, CCM.

Mwandishi wa alijaribu kuzidaka pointi muhimu  anazotoa  Mwigulu Nchemba (Zinaanzia  chini  kuja  juu) alipokuwa akitangaza nia yake;

25: Mh. Mwigulu tayari amemaliza kuzungumza na sasa anaendelea kufurahi na watu walioko ukumbini. Kinachofuata  kwa  sasa  ni  maswali  mbalimbali  ambayo  ataulizwa  na  kuyajibu.

24: Mambo matatu ninayowaomba Watanzania ni kwamba mniamini, pili mniunge mkono na tatu nitawavusha. 

23: Natangaza rasmi kuomba ridhaa ya kugombea katika chama changu ili niweze kuleta mabadiliko Katika Nchi yangu. 
  
22: Napoenda kupigana vita hii siendi kupigana kwaajili ya Watanzania ila mimi mwenyewe maana umaskini unanigusa. 

21: Ukiwaondoa vijana mjini wakati wakifanya kazi halali kwa kigezo cha uchafu,watarudi mjini na kufanya kazi haramu. 
  
20: Tunaposimamia kuacha kufanya kazi kwa mazoea ndio tunasema mabadiliko ni vitendo na wakati ni sasa. 

19: Ninapotangaza nia ya jambo hili nimetathimini vya kutosha na nikajiridhisha na ahadi yangu ni kwamba nitawavusha. 

  
18: Nawaambieni nawaomba kazi hii nikiwa bado nina nguvu ili niweze kufika mwenyewe maeneo yenye migogoro ya ardhi. 
  
17: Tutasimamia Muungano wetu maana sio wa vitu ila ni watu. tutahakikisha uchumi wa Zanzibar nao unapewa kipaumbele. 
  
16: Mtu anayeiba dawa ambazo zingemtibu maskini huyo ni mhujumu, tutamnyang'anya leseni yake na atakwenda jela. 
  
15: Ninaposema kukomesha rushwa nitazingatia maslahi ya Wafanyakazi, haiwezekani wengine Wale kidogo na wengine kubwa .
  
14: Mtu anabakiza muda mchache hadi anakuja kustaafu unamuongezea muda tena kazini wakati kuna vijana wasio na kazi. 
  
13: Mtu yoyote akithibitika amefanya vitendo vya rushwa, atafilisiwa, atafukuzwa kazi na atafungwa. 
  
12: Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na rushwa hurudisha nyuma maendeleo. 
  
11: Awamu ya 5 nataka kuona nchi ikiingia kwenye uchumi wa viwanda na vijana wakifanya kazi kwa shift usiku na mchana .
  
10: Pia jambo lingine la kuzingatia ni Udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. 

9:Mambo ya kuzingatia ni Kila mtu kulipa kodi anayostahili na sio kukandamiza wafanyakazi na kinamama wauza vitumbua .

8:Mkataba wa Rais wa awamu ya tano ni juu kazi anazoenda kufanya na sio kazi alizowahi kufanya.  


7: Faida  ya  kuwa  kiongozi  Kijana  ni  kuwa Unafanya kazi ukiwa na nguvu na ukimaliza unapumzika, kwahiyo unajiuliza tena hilo? 
  
6: Kiongozi akipatikana kwa mazoea, atafanya kazi kwa mazoea. Nawaambieni tunataka tukomeshe kufanya kazi kwa mazoea

5: Kukaa sana serikalini si kigezo, unaweza kukaa sana serikalini na ukawa umesababishia hasara kubwa Taifa hili. 


4: Nilipomaliza shahada ya 2  nilibeba zege na mke wangu alipika mama ntilie, natambua tatizo la ajira kwa vijana. 

3: Kiongozi aliyekaa muda mrefu madarakani maana yake ni kwamba amesahau shida za wananchi. 

2: Nimeamua kutangazia nia Dodoma kwakuwa ni Makao makuu ya Nchi na pia makao makuu ya chama.
 


1: Namshukuru MUNGU kwa kuniwezesha leo kusimama mbele yenu kwaajili ya kutangaza jambo kubwa kwaajili ya nchi yetu .

No comments