NINI TATIZO DULLAH MJUKUU WA AMBUA NA PLANET BONGO KUTOKA EATV
Siku ya kesho itakua mbaya sana kwa mashabiki wa show pendwa sana na vijana kutoka ting'a nambari wani nchini Tanzania kutokana na taarifa za kufika ukomo kwa show hiyo.
Dullah kupitia E-news aliwashukuru mashabiki wa kipindi hicho kwa kuwa naye kwa muda wa miaka saba tangu alipokabidhiwa mikoba hiyo na mwanadada maarufu Salama Jabir ambaye kwa sasa anaendesha kipindi cha Mkasi ambacho hufanya mahojiano na watu mbalimbali maarufu hapa nchini.
Kupata full stori kuhusiana na kufika ukomo kwa show hiyo usiache kusikiliza East African Radio siku ya kesho ambapo atajumuika na mkongwe wa show hiyo Salama pamoja na Dj Kim kuanzia saa nne hadi sita ili uweze kujua nini sababu ya kufika ukomo kwa show hiyo
No comments