Habari mpya

WIMBO WA IZZO BUSINESS X-MASS WAMKUNA DJ CHOKA - MR. APETITE

DJ Mzoefu na Blogger DJ Choka leo amefunguka baada ya kusikiliza mkwaju mpya wa Izzo Bizness  Mr Xmass na Kuguswa na moja ya line ya track hiyo.

NAOMBA KUZUNGUMZA HIKI.

"Nimesikiliza wimbo mpya wa @izzo_biznesss zaidi ya mara kumi na kuna #LINE nyingi kaziimba lakini mstari huu ndio umenigusa. "TUMEPANDA GARI MOJA TUMELIPWA TOFAUTI"
Hii line imenigusa KINOMA kwasababu ninauzoefu wakuwa kwenye TOUR BUS muda mrefu sana nikiwa na wasanii wakubwa wa hapa nyumbani na nimeshasafiri TOUR zote kubwa hapa TANZANIA.

Kuna tour nyingine wasanii wanalipwa kwa kumwangalia msanii, utasikia ananyimbo ngapi Huyu basi alipwe hivi, utakuta msanii mkubwa hapa bongo anawekwa kwenye show moja na hawa wasanii wadogo ambao husema wamepewa hela nyingi kwasababu anahit song kwa wakati huo.

Chaajabu msanii aliyepewa hela nyingi anaenda kuboronga lakini anayelipwa hela ndogo bora mradi liende yeye ndio anaenda kuwarusha mashabiki KINOMA NOMA. Kinachokuja kuendelea msanii mdogo analeta dharau na kuanza kusema hawa wakongwe wameshachuja. Kinachowafanya wawe vile ni kwasababu nyie waandaaji mnawaweka KIMATABAKA, Wasanii fulani walale HOTEL ile na hawa walale hotel ile pale, unadhani kutakuwa na nini hapo.

Wasanii wa BONGO wangekuwa wanalipwa sawa kwenye show zao za TOUR ingeleta maana sana halafu hili neno ya kwamba mimi nalipwa zaidi kuliko msanii mwingine iwe kwenye zile show zao moja moja wanazopiga mikoani au kwenye vimeo vyao vingine vyakutafutia UGALI.

#NIMEMALIZA" Alisema DJ Choka.

No comments